Meneja Maduka, Chakula na Huduma wa Kampuni ya Total nchini Tanzania Jane Mwita akitoa zawadi ya ua kama ishara ya upendo kwa wateja wao ambao wamefika kujaza mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Total cha Mliman City jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo imeamua kusambaza upendo katika siku ya Valentine.
Meneja wa Kituo cha Mafuta cha Total Mliman City jijini Dar es Salaam Luqman Salum akitoa zawadi ya ua kwa mteja wao ambaye amefika kujaza mafuta kwenye kituo hicho leo siku ya Valentine Day.Kampuni ya Total imeamua kutoa zawadi hiyo kama ishara ya upendo kwa wateja wao.
Meneja Maduka, Chakula na Huduma wa Kampuni ya Total nchini Tanzania Jane Mwita akiwa ameshika maua ambayo ni zawadi kwa ajili ya wateja wao kama ishara ya kusambaza upendo katika siku ya Valentine.
Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Kampuni ya Total Tanzania Marsha Msuya (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa siku ya Kusambaza Upendo katika Siku ya wapendanao ambapo kampuni ya Total wameshirikiana na Kampuni ya Coca cola kuandaa zawadi maalumu kwa ajili ya wateja wao hasa wanawake ambao watakuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyekundu.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Coca cola Kanda ya Dar es Salaam Ruqaiya Alibhai pamoja na Meneja Msimamizi wa Maduka , Chakula wa ToTAL Jane Mwita. Hafla hiyo imefanyika leo katika Kituo cha Mafuta cha Total cha Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Kampuni ya Total Tanzania,Marsha Msuya (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mteja wa kwanza aliyefika katika kituo cha Total Mliman City Sarah Ndile wakati wa siku ya Kusambaza Upendo katika siku ya wapendanao ambapo kampuni ya Total wakishirikiana na kampuni ya Coca cola wametoa zawadi maalumu kwaajili ya wateja wao hasa wanawake.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Coca cola Kanda ya Dar es Salaam Ruqaiya Alibhai pamoja na Meneja Msimamizi wa Maduka , Chakula wa Total Jane Mwita
Zenah Mungai kutoka Kampuni ya Mafuta ya Total akimuwekea bango lenye ujumbe wa Sambaza Upendo mteja wao Leila Hassan ambaye alikuwa amefika katika Kituo cha Mafuta cha Tofal Mliman City kujaza mafuta.


Na Mwandishi Wetu, Michuzi Globu ya jamii

KAMPUNI ya Mafuta ya Total imeungana na Watanzania kusherehekea sikuku ya wapendanao ya Valentine kwa kuhamasisha upendo ambapo imetumia siku hiyo ya Februari 14 kutoa zawadi kwa kwa kila mteja mwanamke aliyefika kuweka mafuta katika kituo cha Total.

Akizungumza kuhusu kuhamasisha upendo, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Total Marsha Msuya Kileo amesema kampuni ya Total inawapenda Watanzania na ina upendo siku zote ndio maana inawaletea mafuta bora yenye kiambata cha excellium na bidhaa bora za vilainishi.

Amesisitiza kampuni hiyo imeamua kuwaonesha upendo kwa kuwapatia zawadi ya sikukuu ya Wapendanao ya Valentine kwa wateja wao, kwa kuonesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea siku hiyo.

"Lengo la kutolewa kwa zawadi hizo ni ishara ya upendo na tumeamua kusambaza upendo kwa wateja wetu wote. Tumeamua kuwahamasisha Watanzania kuwa na upendo kwa kupendana kama Total inavyowapenda Watanzania, na tunawakumbusha kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha Total, haujazi mafuta tuu, bali unajaza mafuta ya Total Excellium ambayo ni mafuta yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo, kwa kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo, yakiboresha injini ya gari yako,"amesema.

Amefafanua jumla ya vituo 16 vya mafuta vya Total ndivyo vimeteuliwa kuendesha zoezi hilo, katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro.

Kuhusu Total amesema ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi na kwamba ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati hiyo duniani kote na inawafanyakazi 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Pia Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.

Baadhi ya wateja ambao wamepata upendo wa Total wameipongeza kampuni hiyo kwa kuonesha ishara ya kuwapenda kwa kuwapa zawadi hiyo na kueleza ni jambo ambalo linawaunganisha kati yao na kampuni hiyo.

Kwa upande wa mmoja wa wateja waliojaza mafuta katika kituo cha Total kilichopo Mliman City jijini Dar es Salaam Leila Hassan amesema hakutarajia kupata zawadi kutoka Kampuni ya Total ikiwemo ya ua lenye rangi nyekundu ambalo ni ishara ya upendo katika siku ya Valentine.

"Tunawapongeza Total kwa kuonesha maana halisi ya Valetine Day kwa vitendo, zawadi ambazo wametoa kwa wateja itabaki kuwa kumbukumbu ya muda mrefu maishani kwetu,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...