Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akikata utepe kuzindua uandikishwaji
wa madereva bajaji kuweza kukata bima ya afya ambapo wamedhaminiwa na
kampuni ya maziwa ya Asas ambapo mkurugenzi wake Ahmed Salim Abri akiwa
pembeni mwa kushoto kwal Lukuvi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimkabidhi cheti cha Shukrani
Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya maziwa ya Asas, Ahmed Abri mara
baada ya kukabidhi bajaji 40 kwa kikundi cha umoja wa madereva bajaji
mkoa wa Iringa (Picha na Denis Mlowe).

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwa na Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya maziwa ya Asas, Ahmed Abri na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakijaribu moja ya bajaji 40 ambazo zimetolewa kwa mkopo kwa Umoja wa madereva bajaji mkoa wa Iringa (UMBI) na kudhaminiwa na kampuni ya maziwa ASAS
*****************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
KAMPUNI ya Asas Group ya mjini
Iringa imekidhamini kikundi cha Umoja wa Madereva Bajaji Iringa (UMBI)
na kufanikiwa kupata mkopo wa bajaji 40 zenye thamani ya Milioni 280 kwa
lengo la kukopeshana na kurudisha ndani ya mwaka mmoja.
Mkopo huo uliotolewa na Finca
Microfinance Bank umekabidhiwa juzi na Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi mbele ya mlezi wa kikundi hicho,
Mkurugenzi Uzalishaji wa Maziwa ya Asas,Ahmed Salim Abri ikiwa ni
udhamini wa kampuni hiyo kulipwa na wanufaika wa bajaji hizo katika
kipindi cha miezi 12 kuanzia sasa kwa kupitia umoja wao huo.
Licha ya udhamini huo
Mkurugenzi huyo, amewawezesha udhamini, amewaahidi kuchangia kiasi cha
sh. 50,000 kwa madereva bajaji 100 kwa ajili ya kuwakatia leseni na wao
kuongeza 20,000 kati 70000 zinazohitajika katika ukataji wa leseni na
kuwakatia bima ya afya.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
bajaji hizo, Ahmed Salim Abri alisema awali aliwataka madereva hao
kupeleka majina ya madereva 100 kwa ajili ya kuwalipia leseni lakini
madereva hao walishindwa hivyo wakati huu amewasisitiza zaidi kufikisha
majina hayo aweze kuwaongezea gharama za leseni ni Sh 70,000 na kutoa
50000 na madereva hao kuchangia 20,000 ili aweze kupata leseni.
Alisema kuwa licha ya
kuwasaidia madereva hao, ameweza kuwadhamini chama cha walemavu mkoa wa
Iringa kupata bajaji 1 na kutoa milioni 1 za kuwadhamini na kufanikisha
upatikanaji wa bajaji hiyo kwa ajili kufanya biashara na kuongeza kipato
kwa chama hicho.
Aidha aliwapongeza madereva
hao na akawataka wazingatie sheria zote muhimu zikiwemo za barabarani
wakati wakitumia vyombo hivyo kuepuka mgongano na kikosi cha usalama
barabarani.
Akikabidhi bajaj hizo, Waziri
Lukuvi aliipongeza kampuni ya Asas kwa udhamini wake kwa madereva hao na
kumpongeza Ahmed Abri kwa kuweza kuwasaidia vijana katika changamoto ya
ajira kwa kupitia biashara ya bajaji na kuwafanya kuweza kujitegemea
lakini pia kuendana na falsafa ya Rais Dk John Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
Aidha Lukuvi alitoa wito kwa
mkurugenzi huyo kuwaangalia madereva bajaji wa jimbo la Ismani na
kuwawezesha kupata mkopo wa bajaji ambapo alisema kwamba bajaji zaidi
zinahitajika kuweza kuwakopesha hadi kufikia idadi ya bajaji 100.
Awali mwenyekiti wa UMBI
Norberth Sunka alisema tangu kuanzishwa kwa umoja wao miaka mitatu
iliyopita wamekwishapata mikopo ya zaidi ya Sh Milioni 670
zilizowawezesha kupata bajaj zaidi ya 95 na kuzikopeshwa kwa wanachama
wake.
Alisema kuwa walianza na mkopo
wa bajaji 9 ambazo walikupoeshana wanachama wa UMBI kwa gharama ya
milioni 50 ambapo walifanikiwa kulipa kwa wakati na kwa kupitia udhamini
wa kampuni hiyo wamekwisha kupeshwa bajaji 97 ambazo zimewakomboa
kuondokana na kuajiliwa.
Sumka alisema Wanachama 40
ambao awali walikuwa madereva wa bajaji za watu wengine wamenufaika na
mkopo huo na kuwawezesha kumiliki bajaji zao wenyewe kutokana umoja wao
ambao umekuwa wepesi kulipa mikopo hiyo ndani ya wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...