Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert
A. Ibuge akipokea baadhi ya nyaraka za Ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe. Makabidhiano hayo
yamefanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert
A. Ibuge akimpa mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji
K. Mnyepe mara baada ya makabidhiano rasmi ya ofisi.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert
A. Ibuge akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Ramadhani
Mwinyi baada ya kumtembelea ofisini kwake leo katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb)
akiwa na Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge alipomtembelea Ofisini
kwake leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
……………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert
A. Ibuge amekabidhiwa Ofisi rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06
Februari, 2020. Kabla ya uteuzi huo Balozi Kanali Ibuge alikuwa Mkuu wa
Itifaki (Chief of Protocol).
Aidha, Balozi Ibuge anachukua
nafasi ya Dkt. Faraji K. Mnyepe ambaye alihamishwa wizara kwa kuteuliwa
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Dkt.
Mnyepe amechukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye amestaafu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...