KIWANDA cha Shelys Pharmaceuticals Ltd cha Mwenge jijini Dar es Salaam chaibuka kidedea katika shindano la nne la KAIZEN lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza wakati wa kuwapa tuzo za ushindi wa kiwanda bora za KAIZEN jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara, Riziki Shemdoe amesema kuwa kiwanda kilichoshinda kitatuwakilisha katika mashindano ya KAIZEN kwa nchi za Afrika zitakazofanyika Mwakani 2020 nchini Afrika Kusini.

"Sisis kama Shelys Pharmaceuticals LtdMwakani tutawakilisha nchi yetu katika mashindano ya KAIZEN kwa nchi za Afrika, huku tukimuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuiandaa Tanzania Kuwa Tanzania ya Viwanda." Amesema Shemina.

Amesema mashindano hayo yanawawezesha wenye viwanda kujulikana ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi.

"Lengo la Mashindano haya ni kuongeza ubora na tija katika uzalishaji wa viwandani pamoja na kuondokana na gharama zisizo za lazima na kuongeza ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi." Amesema Shemdoe.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kiwanda cha Dawa cha Sherlys (Shelys pharmaceutical LTD), Shemina Somji amewashukuru wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuanzisha shindano la KAIZEN.


Mashindano ya KAIZEN hapa nchini yamekuwa yakifanyika kila mwaka ifikapo Februali, 18 ingawa hapa nchini KAIZEN imeanza kuenea 2017.


 KAIZEN ni falsafa kutumia mbinu bunifu ya uimarishaji endelevu wa tija ya ubora viwandani ambayo inazingatia usimamizi na matumizi bora ya rasilimaliwatu, fedha, muda na miundombinu ili kupunguza upotevu wa gharama zisizokuwa na lazima viwandani na hatimaye viwanda kuweza kuhimili ushindani wa biashara.

Wawakilishi wa kiwanda cha Kiwanda cha Shelys pharmaceutical LTD cha Mwene jijini Dar es Salaam wakipokea tuzo mara baada ya kushinda shindano la KAIZEN lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Kiwanda cha Dawa cha Shelys (Shelys pharmaceutical LTD), Shemina Somji akipokea cheti cha Ushiriki wa mashindano ya KAIZEN jijini Dar es Salaam leo.
Washiriki wa shindano la KAIZEN wakiwa na tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki wa shindano hilo.






























 Baadhi ya washiriki wa shindano la nne la KAIZEN wakipokea vyeti vya ushiriki leo katika sherehe za kukabidhi mshindi tuzo.
 Mkurugenzi wa Biashara wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Leo Lyayuka akizungumza leo wakati wa kukabidhi tuzo za KAIZEN jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...