Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo
Februari 22, 2020 ameondoka mkoani Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya
kikazi ya siku moja. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akiwaaga viongozi
kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel
Maganga kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya
siku moja mkoani humo, Februari 22, 2020. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
CCM wa mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama ngoma kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kabla ya kuondoka
baada ya kukamilisha ziara ya siku moja mkoani humo, Februari 22, 2020.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...