Wakati taharuki ya mafuriko mkoani Lindi ikiendelea,Mbunge wa kuteuliwa na Rais Mama Salma kikwete na mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne amefika mkoani Lindi na kuongozana na viongozi wa chama cha mapinduzi kwenda kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko.

Katika ziara hiyo Mama Salma kikwete amefika katika kambi ya Nanjime na mji mwema yenye jumla ya Waathirika 482 na kuwafariji.

"Kwa niaba ya wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali na chama cha mapinduzi walinipatia salamu za pole ili nizifikishe kwenu, tunaungana kuwapa pole na kuwahakikishia kuwa tuko pamoja nanyi kwa hali na mali katika wakati huu mgumu mnaoupitia"

"Niwaombe saana wadau mbalimbali,viongozi, wafanyabiashara na yeyote aliyeguswa kujitoa kwa moyo kuwasaidia ndugu zetu hawa walio kwenye hali mbaya hivi sasa"

Sambamba na salamu hizo za pole, Mama Salma kikwete amekabidhi vifaa vya kuwasaidia wathirika hao wa mafuriko Bati 500, Doti za kanga 100,Matrubai,viatu pea 50, sabuni Miche 50,Miswaki na dawa za Meno,Nguo za kiume na chakula katika ofisi ya mkuu wa wilaya.

Akiongea katika kambi hiyo mganga Mfawidhi wa kituo cha kitomanga Dr.Gidion Kategugwa ameishukuru serikali ya mkoa kwa jitihada wazozionyesha kwa kuleta Dawa kwa wakati yanayowarahisishia kutibu wagonjwa huku akisema changamoto walionayo ni magonjwa ya matumbo na malaria kwani changamoto ya Vyandarua ni kubwa hivyo ameiomba serikali na wadau mbalimbali kufanya jitihada za haraka za upatikanaji wa Vyandarua kwa Waathirika hao.

Kwa upande wa wawakilishi wa Waathirika hao,Bwana Bakari Issa Mkulang'ombe Mkazi wa Kijiji cha mkwajuni kitongoji cha Nanjime Ameishukuru Serikali kwa jitihada za kuwaokoa na kuiomba serikali kuwasaidia kwa haraka huduma ya chakula,Maturubai ,mavazi na chakula huku akiomba serikali kuwapatia mbegu za mazao ya muda mfupi ili waweze kujikwamua kwa baadae.

Nae Fatuma Ismail Nantima amewaomba wadau kuwasaidia mavazi kwa wakina mama na sare za shule kwa watoto ili waweze kuendelea na masomo wakati jitihada zingine zinaendelea.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...