Na Amiri Kilagalila,Njombe
Waziri wa maji Prof.Makame Mbalawa ameagiza kuwekwa kizuizini msimamizi wa ujenzi wa mradi wa maji wa Igando Kijombe unaotekelezwa na kampuni ya  STC JV YELL LMT wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe Erick Mlema kwa kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati.

Waziri Mbalawa  amesema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 17 pekee huku wananchi wakilalamikia kero ya upatikanaji wa maji wilayani humo.

Mradi wa Igando- kijombe unatajwa kugharimu takribani billioni 12 na ulianza rasmi mwaka 2018 mwezi wa 10 na kutakiwa kukamilika mnamo mwezi wa kumi 2019 na kulazimika  kuongezewa muda mkandarasi huyo mpaka mwezi wa 4  2020.

“Katika mkoa wenye changamoto kubwa za miradi ya maji ni Njombe,kuna mradi huu ambao unafika asilimia 17 hata tukimuongezea muda hamalizi,kuna mradi Makambako umefika asilimia 2 na ni mradi wa bilioni 6 hakuna kitu”alisema waziri Mbalawa

Mbalawa amesema kutokana na hali hiyo,miradi yote yenye shida serikali itawafuta wakandarasi na kuichukua ili kuwatekelezea wananchi na kuwasaidia kuwafikishia huduma.

Mbunge wa jimbo la Wanging’ombe Gerson Lwenge amesema mradi huo tangu kuanza kwake umekuwa na shida kubwa na kulazimika kumuomba waziri kuanza kulifanyia uchunguzi suala la kusua sua kwa mradi huo kuanzia kwenye wizara.

“Maradi huu toka mwanzo ulikuwa na matatizo ndio maana unakuta bei zinaleta shida,lakini la msingi tutafute kila namna inayowezekana ili wananchi wetu hawa mradi uweze kukamilika”alisema Lwenge

Baadhi ya wananchi wilayani humo akiwemo Osca Kilamya wanasema ni shauku yao kuona mradi unaanza kufanya kazi ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...