Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Daniel Budeba  (kushoto) ametembelea banda la GST katika maonesho ya  kimataifa ya uwekezaji sekta ya madini Tanzania yanayofanyika katika ukumbi wa Julius Kambarage Nyerere jijin Dar es Salam. Dkt. Budeba ameipongeza timu ya GST kwa ilivyojipanga katika kuwahudumia wadau mbalimbali wanaotembelea banda la GST. 

Aidha, kupitia maonesho hayo Dkt.Budeba amepata fursa ya kufanya mazungumzo na wawekezaji mbalimbali na kuwaeleza fursa ya madini zilizopo Tanzania. Vilevile, Dkt. Budeba amewaeleza wawekezaji hao kuwa GST ipo tayari kuwapa ushirikiano kwa kuwapatia taarifa za jiosayansi wanazohitaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini. "GST ni mhifadhi mkuu na pekee kwa niaba ya Serikali wa taarifa za jiosayansi zinazoonesha  madini yanayopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi", aliongeza Dkt. Budeba.  GST inashiriki Mkutano na Maonesho ya kimataifa ya uwekezaji katika sekta ya madini yanayofanyika kuanzia tarehe 22 - 23/02/202 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...