Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akikabidhi kombe kwakiongozi wa timu ya mpira wa pete, Bi. Kuruthumu Kudra
baada ya timu ya MNH kuichabanga timu ya Muhimbili-Mloganzila mabao 16-11. Kushoto ni Kaimu NaibuMkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth
Magandi.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Muhimbili-
Mloganzila wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali yaTaifa (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akikabidhi kombe kwakiongozi wa timu ya kuvuta Kamba ya Muhimbili-Upanga,
Bw. Ali Lidenge baada ya timu ya wanaume na wanawakekuichabanga timu ya kuvuta Kamba ya Muhimbili-Mloganzila.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Upanga, Prof.Lawurence Museru akisalimiana na kiongozi wa timu yampira wa pete ya MNH, Bi. Kuruthumu Kudra kabla ya
kuanza kwa mpira huo.
Wanchezaji wa Muhimbili-Upanga na Mloganzila
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao.
****************************
Na Sophia Mtakasimba.

Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila
imeinyuka Timu ya soka ya Muhimbili-Upanga mabao 3-1
wakati timu ya mpira wa pete ya Muhimbili-Upanga
imeichabanga Muhimbili-Mloganzila mabao 16- 11 katika
Bonanza la michezo lililofanyika Viwanaha vya JMK PARK
jijini Dar es Salaam.

Mchezo huu ulionekana kuwa na upinzani mkubwa huku
Muhimbili-Upanga wakionyesha kandanda safi na kujipatia
bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza.

Baada ya wachezaji wa Muhimbili-Mloganzila kupachikwa
bao walikuja juu na kulishambulia lango la Muhimbili-
Upanga na kujikuta wakijifunga na hivyo na mabao kuwa
1-1 katika kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili kila timu ilionyesha kukamiana huku,
Muhimbili-Upanga ikiishambulia kwa kasi timu ya
Muhimbili-Mloganzila, lakini bahati haikuwa yao kwani
walionekana kukosa nafasi nyingi za wazi.

Muhimbili-Mloganzila zikiwa zimebaki dakika 10
kumalizika kwa mchezo, ilibadilisha upepo kuwacharaza
wapinzani wao mabao mawili ndani ya muda huo na hivyo
ubao wa matangazo kusomeka mabao 3-1.

Bao la timu ya Muhimbili-Upanga lilipachikwa wavuni
kupitia mshambuliaji wake hatari, Abdalah Laiser wakati
mabao ya Muhimbili-Mloganzila yalifungwa na Abdul
Hamad, Omary Koppy na bao la tatu lilipachikwa wavuni
na Steven Wiligis.

Katika hatua nyingine, timu ya Kamba ya Hospitali ya
Taifa Muhimbili-Upanga ya wanaume na wanawake kila
moja wameshinda mabao 2-0 dhidi ya timu ya Kamba ya
wanaume na wanawake ya Muhimbili-Mloganzila.

Baada ya kupatikana kwa ushindi huu, mashabiki wa
Muhimbili-Upanga waliinuka kwenye viti na kuanza
kushangilia ushindi huu huku wakisema ‘wameicharaza
timu Muhimbili-Mloganzila hivyo waende kujifunza mchezo
wa kuvuta Kamba.’

Akizungumza baada ya michuoano hiyo, Mkurugenzi wa
Huduma za Tiba wa Muhimbili-Upanga, Dkt. Hedwiga
Swai amewashukuru watumishi kwa kujitoa katika
michezo kwani lengo si kutafuta ushindi bali kudumisha
uhusiano na upande uliopo kati ya Muhimbili-Upanga na
Muhimbili-Mloganzila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...