Na, Geofrey A. Kazaula
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege ameelezea kuridhishwa kwake na miradi ya barabara iliyotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tarura katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza ambapo ameeleza kuwa mafanikio yanayopatikana katika Manispaa hiyo hasa katika miradi ya barabara yanatokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wataalam wa TARURA na watumishi wengine wa Manispaa kwa kufanya kazi pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.

‘‘ Wote tumeshuhudia barabara hizi zilivyo kwenye kiwango, mafanikio haya yanatokana na Umoja uliopo kwa watumishi wote wa Manispaa ya Ilemela pamoja na watumishi wa TARURA kwani wanafanya kazi kwa pamoja ili kuwaletea wananchi wetu maendeleo, kiujumla wanafanya vizuri’’Kandege.

Aidha amesisitiza kuwa miundombinu ya barabara inapokamilika ilindwe kwa nguvu zote na amewaagiza viongozi husika huhakikisha barabara hizo zinafanyiwa usafi mara kwa mara na kulinda miundombinu ya barabara hizo.

Naye Meneja wa TARURA Manispaa ya Ilemela Mhandisi Clement Kihinga amesema kuwa barabara hizo zilizotekelezwa chini ya mradi wa Tanzania Strategic Cities Project (TSP) zimekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuinua uchumi wa wananchi na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanailinda miundmbinu ya barabara ilizidumu na ziendelee kuboresha maisha yao na kurahisisha suala la usafiri na usafirishaji katika Manispaa ya Ilemela.

‘‘Serikali inatumia gharama kubwa sana kujenga barabara hizi hivyo nitoe wito kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kulinda miundombinu hii ya barabara ’’ amesema Mtaalam huyo.

Mmoja wa wananchi wa Kiseke A Ilemela Issa Shabani alisema awali usafiri ulikuwa changamoto sana Katika barabar yao kwani miundombinu ilikuwa mibovu sana ila baada ya baraba ya kiseke Busweru kukamilika maisha yamepanda kiuchumi

“Sasa nafanya biashara yangu ya matunda hapa Busweru, nayabeba salama na hayaharibiki kwani barabara ni nzuri na hata kipato changu kimeongezeka hivyo naishukuru sana Serikali kwa kujenga barabara hii”Alisema Shabani.

Ziara ya Kandege inaendelea Mkoani Mwanza ambapo miradi mbalibali ya maendeleo zikiwemo barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA inatarajiwa kukaguliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...