Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Nchini, Mh. Atashasta Nditiye Ijumaa ya tarehe 28 Februari, 2020 amehitimisha Kampeni maalum ya Shirika la Mawasiliano Nchini, TTCL ijulikanayo kama “SWITCH-ON, Mawasiliano kwa wote” kwa mikoa ya Ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania katika kijiji cha Irkuishbor wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

Kampeni hiyo iliyoambatana na zoezi la kuzindua Minara ya Mawasiliano ya Shirika hilo kwa ukanda wa Kaskazini ilianzia Jijini Tanga tarehe 25 Februari, 2020 na kuendelea katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na kuhitimishwa Mkoani Manyara.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano nchini, Bw. Waziri Kindamba, Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bi. Puyo Nzalayaimisi na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa ngazi za Mkoa wa Shirika hilo kubwa la Mawasiliano.

Mh. Nditiye alisema Kampeni hii itaendelea sehemu mbalimbali nchini ambazo zina changamoto ya mawasiliano, “Nimeshiriki katika ziara hii ya kampeni ya SWITCN-ON, Mawasiliano kwa wote, ambayo inasimamiwa na TTCL Corporation katika mkoa wa Morogoro, Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Nilizindua rasmi kampeni hii katika kambi ya kikosi 121 Mkoani Morogoro Kidugala Sangasanga, baadaye nikazindua Mnara wa Mawasiliano katika kata ya Masalai Muheza Tanga, Kashashi Siha Kilimanjaro, Mundarara Longido Arusha na hatimaye kuhitimisha katika wilaya hii ya Kiteto, Manyara na tutaendelea na zoezi hili Nchi nzima kuweza kuwafikia wananchi wote”.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Nchini, Mh. Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa TTCL katika kampeni ya  “SWITCH-ON, Mawasiliano kwa wote” katika kijiji cha Irkuishbo wiliyani Kiteto mkoani Manyara.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Nchini, Mh. Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akishangilia pamoja na wananchi wa kijiji cha Irkuishbor, Kiteto Mkoani Manyara mara baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa TTCL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...