Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (wapili kushoto), Mbunge wa Jimbo la
Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omar
Mgumba (wakwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL),Waziri Kindamba wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa
Minara wenye lengo la kufikisha mawasiliano karibu na wananchi,tukio
hilo limefanyika katika kijiji cha Sangasanga, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano, Atashasta Nditiye akizungumza wakati wa tukio la Uzinduzi
wa Minara wenye lengo la kufikisha mawasiliano kwa wananchi. Tukio hilo
limefanyika katika kijiji cha Sangasanga, mkoani Morogoro

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini
Mashariki ambae pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba akizungumza
wakati wa tukio la Uzinduzi wa Minara wenye lengo la kufikisha
mawasiliano kwa wananchi wote.Tukio hilo limefanyika katika kijiji cha
Sangasanga, mkoani Morogoro.

Mkuu wa Kikosi 121 KJ, Luteni
Kanali Abdul Yusuph Ibrahim akizungumza wakati wa tukio la Uzinduzi wa
Minara wenye lengo la kufikisha mawasiliano kwa wananchi .Tukio hilo
limefanyika katika kijiji cha Sangasanga, mkoani Morogoro

Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL), Waziri Kindamba, akizungumza
wakati wa tukio la Uzinduzi wa Minara wenye lengo la kufikisha
mawasiliano kwa wananchi. Tukio hilo limefanyika katika kijiji cha
Sangasanga, mkoani Morogoro.Picha na TTCL
…………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, amezindua Kampeni ya
Uzinduzi wa Minara ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), ambayo
itasogeza mawasiliano karibu na wananchi wa pembezoni mwa miji mikuu,
vijijini na maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na mawasiliano huko nyuma.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika katika kijiji cha Sabgasanga, mkoani
Morogoro ,Naibu Waziri alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Rais Dkt.John Pombe Magufuli imedhamiria kufikisha mawasiliano kwa
ukaribu zaidi ili wananchi waweze kuwasiliana kwa lengo la kukuza
shughuli mbalimbali za kiuchumi.
“Katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita,serikali imekua katika jitihada za kuendeleza
utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali kwa lengo la kuinua sekta
ya mawasiliano ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda” amesema Nditiye
Pia alizungumzia
kukamilika kwa ujenzi wa awamu ya kwanza na pili ya Mkonga wa Taifa
Mawasiliano wenye urefu wa kilomita zaidi ya 7,560 ambao umewezesha
utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi kwa haraka na ubora nafuu
sambamba na kuiwezesha serikali kushusha gharama za mtumiaji wa mwisho.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania
(TTCL),Waziri Kindamba amesema mnara huo uliozinduliwa umegharimu kiasi
cha Shilingi Milioni 261 huku akiwakikishia wananchi juu ya utekelezaji
wa miradi mingine vijijini na maeneo yasiyo na mvuto kibiashara ili
yaweze kuwa na mvuto huo utakaoletwa na athari za mawasiliano huku
akikemea tabia ya uharibifu wa miundo mbinu ya mawasiliano.
“Nitoe rai kwa
wananchi kulinda minara hii ambayo tutaizindua sehemu mbalimbali
nchini,shirika limewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika mradi huu hivyo
si vyema miundo mbinu hii kuhujumiwa kwani nchi itakua imepoteza kiasi
kikubwa cha fedha” amesema Kindamba.
Shirika la
Mawasiliano (TTCL),limekua likishirikiana pia na Mfuko wa Mawasiliano
kwa wote(UCSAF) katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana
kwa Watanzania na pia kuviwezesha vikosi vya majeshi yetu kuwa na
mawasiliano ya uhakikaya simu za mkononi na intaneti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...