Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa Wananchi wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kidumu la mpiga Kura kwa siku mbili zilizo baki.

Zoezi hilo la uandikishaji la daftari la kudumu Mpiga kura linaendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Cosmas Mwaisobwa amesema Wananchi watumie nafasi ya haki yao ya kujiandikisha ili kupiga kura mwaka huu.

Amesema uratibu uliowekwa ni mzuri kwani mtu anatumia dakika tano kupata kadi ya kupigia kura.

Dkt.Mwaisobwa amesema kuwa kwa wale ambao walikuwa na kadi hizo na zikapotea katika mazingira yeyote wafike na kuhakikiwa katika mfumo ili wapate kadi nyingine.

Aidha amesema kuwa siku ziliozobaki Watu wajitokeze wasisubiri siku ya mwisho kwa kuwa na foleni wakati muda upo.

"NEC tumejipanga kwa kuandikisha watu wote na Rasilmali Watu ipo pamoja na vifaa vya kutosha na mtu anapata kadi yake kwa dakika tano"amesema Dkt Mwaisobwa.


Zoezi la uandikishaji  wa Daftari la kudumu la mpiga kura likiendelea kufamyika maeneo mbalimbali jijini Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...