Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT) kimeeleza azma yake ya kuendelea kutoa wataalamu waliokidhi vigezo ili kuweza kuendesha sekta ambazo Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli umewekeza kwa kiasi kikubwa na hiyo ni pamoja na kufufua na kuimarisha shirika la ndege la taifa (ATCL) sambamba na ujenzi wa reli pamoja na meli kubwa katika maziwa makuu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wajumbe wapya wa bodi walipotembelea maeneo ya kujifunzia na vitendo chuoni hapo Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Mhandisi Profesa. Blasius Nyichomba amesema kuwa NIT kikiwa Chuo pekee ya Usafirishaji nchini kimejaribu kubadilisha mfumo wa ufundishaji.
"Asilimia 65 hadi 70 ya ufundishaji chuoni hapa ipo katika vitendo na mazoezi ya mikono kama ni mafundi magari shughuli zao zimejikita katika kazi za mikono na vitendo na tunaamini kuwawezesha wanafunzi kufaulu bila kufahamu vitendo zaidi haitamsaidia, tunahakikisha daraja analolipata linafanana na anachokifanya" ameeleza.
Amesema kuwa mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kujifunzia kwa nadharia na vitendo pamoja na kukutana na wafanyakazi wa chuo hicho watatoka na sauti moja ambayo kwa namna moja au nyingine itasaidia katika kuimarisha na kukipeleka chuo hicho mbele zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Profesa. Zacharia Mganilwa amesema kuwa NIT imeendelea kupiga hatua zaidi hasa kwa kutoa rasilimali watu wenye viwango vinavyokidhi mahitaji ya jamii;
"Tuna jengo ambalo limejengwa na mapato ya ndani ambapo Kuna vituo viwili ikiwemo kituo cha usafiri wa anga na usafirishaji kilianzishwa na benki ya dunia na kinatoa mafunzo kwa marubani, watengenezaji wa ndege, wahudumu wa ndege na masuala ya usafirishaji pamoja na kituo kilichoanzishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kituo ambacho kinaandaa wataalamu watakaosaidia sekta ya barabara ili kupunguza ajali na mchakato ulianza Mei 31 mwaka jana na unaendelea hadi sasa" ameeleza Mganilwa.
Kuhusiana na mafunzo kwa marubani wanafunzi Mganilwa amesema kuwa hadi sasa wamefikia katika mchakato wa ununuzi wa ndege za mafunzo na ndani ya miezi 7 hadi 8 marubani hao watakuwa angani wakipata mafunzo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...