Rais wa klabu ya Paris Saint German (PSG) Nasser Al Khelaifi.

Yassir Simba , Michuzi tv
RAIS wa klabu ya Paris Saint German (PSG) Nasser Al Khelaifi  amehusishwa na makosa ya jinai nchini Swirzerland dhidi ya Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Dunia FIFA Jerome Valcke.

Kupitia mtandao wa habari za kimichezo goal.com umesema taarifa iliyotoka katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Nchini Switzerland imedai kwamba raisi huyo wa klabu ya PSG alimpatia rushwa ya kiasi cha fedha euro million 1.25 Katibu mkuu wa zamani wa FIFA bwana Valcke.

Ofisi hiyo ya mwanasheria Mkuu ya nchini Switzerland imedai Al Khelaifi alimpatia kiasi hicho cha fedha bwana Valcke ili ampatie haki ya kurusha matangazo ya fainali za kombe la dunia kati ya mwaka 2018 na 2030 zitazofanyika nchini Qatar ikiwa pamoja na matukio ya kimichezo ya shirikisho hilo.

Pia inadaiwa Nasser Al Khelaifi ni mmiliki kituo cha utangazaji wa habari za kimichezo cha Bein Sports.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...