RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitia mchanga katika kaburi lililokuwa na
mwili wa Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu
Zanzibar Jaji Mkusa Sepetu , wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijiji kwao
Mbuzini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 16-2-2020(

RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Amani Karume na Wauminiu wa Dini ya
Kiislam, wakiitikia dua baada ya kumaliza kuusalia mwili wa Marehemi
aliyekuwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar. Mkusa Sepetu, iliofanyika
katika Msikiti wa Ijumaa Mbuzini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.(Picha
na Ikulu)

RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
akijumuika na Viongozi na Wananchi katika kisomo cha hitma kumuombea
Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe. Mkusa Sepetu kabla ya
kuusalia mwili wa marehemu katika Msikiti wa Ijumaa Mbuzini Wilaya ya
Magharibi “A” Unguja (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Hassan Othman Ngwali na (kulia kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar
Mhe, Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali
Maulid na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said.(Picha na
Ikulu)

RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
na (kushoto kwa Rais ) Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Amani Karume
na Viongozi na Wananchi mbalimbali wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh
Fadhil Soraga baada ya kumalizika kwa maziko ya Jaji wa Mahkama Kuu
Zanzibar Marehemu Jaji Mkusa Sepetu, yaliofanyika Kijiji kwao Mbuzini
Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...