
************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda leo February 18 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi
wa Uturuki Nchini Tanzania Mhe. Ali Davulaglu, Balozi wa Tanzania Nchini
Uturuki Prof.Elizabeth Kiondo, Mstahiki Meya kutoka Uturuki, Wawekezaji
na Wafanyabiashara zaidi ya 40 kutoka Nchini Uturuki waliokuja Kutazama
na kuchangamkia fursa za Uwekezaji wa Viwanda jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo RC Makonda
amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mkoa huo itawapatia
ushirikiano wa kutosha wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza ili kutimiza
malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.
Aidha RC Makonda amewaeleza
wawekezaji hao kuwa Jiji hilo linajivunia kuwa na Amani na Utulivu
pamoja na fursa ya uwepo wa Bandari, Uwanja wa Ndege pamoja na
Miundombinu yote muhimu ya kuvutia Uwekezaji.
Hata hivyo RC Makonda amesema
February 20 atawapeleka wawekezaji hao Wilaya ya Kigamboni ili
wakajionee maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji wa Viwanda huku
akimshukuru Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki Prof. Elizabeth Kiondo kwa
kuwaleta wawekezaji hao.
Nae Balozi wa Uturuki nchini
Tanzania Mhe. Ali Davutaglu amemuhakikishia RC Makonda kuwa Uturuki
itazidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Tanzania katika nyanya
mbalimbali za maendeleo na wamemualika RC Makonda kwenda kutembelea Nchi
ya Uturuki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...