Afisa Utalii wa
Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa
habari
| Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo akielezea mikakati waliokuwa nayo |
| Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei akizungumza kuhusu namna walivyonufaika na uwepo wa hifadhi hiyo |
| Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae katikati akiwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo |
| Sehemu ya wageni wakifurahia utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan |
![]() |
| Aina ya malazi yanayopatikana kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa wageni wanaofika kutembelea vivutio mbalimbali |
| Mamba akiwa pembezoni mto Wami akiota jua kama alivyokutwa ambapo jamii ya Mamba wanapatikana pia kwenye hifadhi hiyo |
Kundi la
Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Saadan
Wanyama
aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Saadan
Aina
ya Makundi ya Ndege ambayo yamejenga kiota kwenye hifadhi ya Taifa ya
Saadan ndani ya Mto Wami ambapo ndege hao huishi pamoja ambao huishi
hapo kwa ajili ya kuijepusha na maadui zao
Wanyama aina ya
Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
Wanyama
aina ya Twiga wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Saadan
Wanyama
aina ya Ngiri wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Saadan
Mnyama
Ngiri akiwa anakula majani karibu na bahari ya hindi kwenye Hifadhi ya
Taifa ya Saadan
Ndege aina
ya Fundi Chuma akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
Mtalii
akifurahia upepo wa bahari ndani ya hifadhi ya Taifa ya
Saadan
Hifadhi
ya Taifa ya Saadani imetumia kiasi zaidi ya sh Bil 1.1 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo kwenye vijiji 11 Kati ya 16 vinavyozunguka hifadhi hiyo kupitia
mpango wa ujirani mwema.
Hayo
yalisemwa na Afisa utalii wa hifadhi hiyo Athuman Mbae wakati akizungumza na
waandishi wa habari walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kujionea shughuli
za utalii.
Alisema
kuwa jumla ya miradi 23 iliyoko kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji na Mazingira
imeweza kufadhiliwa na hifadhi hiyo kwa kushirikiana na
wananchi.
"Tumekuwa
tukishiriki katika miradi ya ujirani mwema ambapo hifadhi inachangia
asilimia 90%
huku wananchi wakichangia asilimia 10% kwa lengo la kuhakikisha wanaweza
kuituza miradi hiyo"alisema Mbae.
Awali akizungumza Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo alisema kwamba alisema maboresho yaliyofanywa kwenye hifadhi hiyo na serikali ya awamu ya tano yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wan je na ndani.
Alisema maboresho hayo yameongeza mwitikio wa watanzania kutembelea hifadhi za taifa kutokana na kuboresha miundombinu ufikaje wake huku watalii wanaweza kufika wakiwemo wa Zanznzar, Dar na Tanga na maeneo mengine hapa nchini.
“Bado tunaendelea kuhamasisha watanzania waone umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini hususani hifadhi ya Kipekee ya Saadani inayopakana na Bahari ya Hindi”Alisema
Kwa
upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei alisema kuwa hifadhi
hiyo imeweza kusaidiana na wananchi katika kutatua kero mbalimbali ambazo
zilikuwa zinatukabili.
"Hifadhi
imeweza kutujengea nyumba ya Mwalimu,kusambaza maji kwenye nyumba za ibada
sambamba na ujenzi wa choo chashule ambacho kilikuwa hakitumiki kwa
muda mrefu kutokana
na uchakavu"alisema Ngulei.
Nao
baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Saadani wamesema kuwa kuishi kwa jirani na
hifadhi kumekuwa ni neema kubwa kwao kwa kipato sambamba na fursa za
biashara.
"Watalii
wengine wakija wanaishi nje ya hifadhi hivyo tunapata kipato kwa kuwauzia
chakula ikiwemo na malazi sambamba na kujifunza tamaduni za kwetu
"alisemaAthuman Said.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...