Mgeni
rasmi wa Tamasha hilo lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Jokate Mwegelo alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jaffo akiambatana na Naibu Waziri
wa Nishati Subira Mgalu na Mbunge wa Viti Maalumu Pwani Zainabu Vullu.
Akizungumza
na wananchi wa Kisarawe , Jaffo amewataka wananchi wa Kisarawe kulinda
miundo mbinu ya maji kwani serikali imetumia gharama kubwa kuweza
kufanikisha mradi huo mkubwa wa maji.
Amesema,
kiasi cha Shillingi bilion 10.6 zimetumika katika kujengwa kwa mradi
huo na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA na kwa sasa
wananchi wa Kisarawe wanapata maji safi kwa muda wote.
"Mradi
huu wa maji umetumia fedha nyingi sana, na maji yanapatikana masaa 24
tuna tenki linalohifadhi lita Milion 6 na mahitaji ya Mji wa Kisarawe ni
Lita milion 1.2 na tayari kuna akiba ya Lita Milion 4.8," amesema.
"Na
kwakuwa tayari maji yapo ya kutosha, nawaagiza Dawasa wamepeleka maji
kwenye maeneo ambayo huduma ya maji safi haijafika na kwakuwa nyinyi ni
watendaji wazuri naamini hilo litafanikiwa,"
Aidha,
Jaffo amesema huduma ya maji imechochea zaidi katika kuboresha huduma
bora kwa wajasiriamali hususani wakina mama lishe ikiwapunguzia gharama
za kununua maji kwa bei kubwa.
"maendeleo
yanakuja kama kuna upatikanaji wa maji na nishati wakutosha, sasa maji
Kisarawe yapo milango iko wazi kwa wawekezaji na pia wakina mama huu
ndio muda wenu wa kutumia fursa"
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kuwa wameamua kuandaa
tamasha la Kisarawe Mamalishe Festival katika kuelekea maadhimisho ya
siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika machi 8 kila mwaka.
Amesema,asilimia
65 ya wanawake wa Kisarawe wanajishughulisha na shughuli ya mama lishe
na lengo likiwa ni kuwakutanisha wakinamama hao ili wabadilishane
mawazo.
"Tukiongelea
katika sekta ya maji, Dawasa wamefanya kazi kubwa sana sasa hivi tuna
mradi mkubwa wa maji na wananchi wanaendelea kuunganishwa tunaishukuru
sana serikali ya awamu ya tano kwa kutuletea maji Kisarawe,"
Meneja
wa Mahusiano Dawasa Everlasting Lyaro ameeleza wanaendelea kuunganisha
wateja wapya na muitikio umekuwa ni mkubwa sana toka mradi huo uanze
kufanya kazi.
Na wamepokea maagizo ya Waziri Jaffo watayatekeleza ili wananchi wote wa Wilaya ya Kisarawe wapate maji safi na ya uhakika.
Wasanii mbalimbali waliweza kuhudhuria akiwamo Shilole, Aunt Ezekiel, Jackline Wolper, Meja Kunta, Sholo Mwamba na wengineo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jaffo akizungumza na wananchi wakati wa Tamasha la Kisarawe Mama Lishe Festival lililofanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wasanii.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na wananchi wakati wa Tamasha la Kisarawe Mama Lishe Festival lililofanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wasanii.
Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe Jokate Mwegelo akionesha zawadi ya vyombo kwa Naibu Waziri wa
Nishati Subira Mgalu na Mbunge wa Viti Maalumu Pwani Zainabu Vullu.watakaokabidhiwa washindi
wa kupika wakati wa Tamasha la Kisarawe Mama Lishe Festival
lililofanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na
wasanii.
Wakina mama Lishe wakiwa wanaendelea na maandalizi ya chakula wakati wa Tamasha la Kisarawe Mama Lishe Festival lililofanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wasanii.
Wakina mama Lishe wakiwa wanaendelea na maandalizi ya chakula wakati wa Tamasha la Kisarawe Mama Lishe Festival lililofanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wasanii.
Picha ya pamoja ya Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI
Selemani Jaffo Mbunge wa Viti Maalumu Pwani Zainabu Vullu, Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na Meneja Uhusiano Dawasa Everlasting
Lyaro na Meneja wa Mkoa wa Kihuduma Kisarawe Ernest Mbwambo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...