Na Immaculate Makilika – MAELEZO
SERIKALI imeandaa programu mbalimbali za kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti zaidi ya bilioni moja katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akijibu swali leo Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Zungu amesema,“Programu ya kwanza ni kupanda miti zaidi ya bilioni moja katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu iliyopo katika nchi yetu, pamoja na kuanza mkakati wa kuomba fedha zilizopo katika Mfuko mpya ulioanzishwa na nchi ya Ufaransa, wa dola za kimarekani bilioni 100, ulioanzishwa kwa lengo la kuboresha mazingira katika nchi zenye uhitaji, ikiwemo Tanzania”.

Aidha, Waziri Zungu aliongeza kuwa mkakati huo wa kupanda miti na kuitunza hivi sasa unaandaliwa katika wilaya zote nchini, na miti itakayopandwa katika kila wilaya itakuwa ya aina maalumu ili kuendana na mazingira yaliyopo katika wilaya husika.

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na asilimia 39.9 ya misitu, misitu hii inapotea, kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2010 tumeshapoteza takribani ekari milioni 8 ya misitu, na hii ni hatari kubwa sana kwa watanzania, tuhakikishe tunaacha kukata miti, tutumie miti kama fursa ya kibiashara, badala ya kuikata tuweke mazao ya nyuki”, amesisitiza Waziri Zungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...