Leo tasnia ya habari nchini hususani redio, inaungana na wanahabari wengine duniani katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Redio Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Februari 13.

Natumia fursa hii kuwapongeza wadau wote wa redio nchini kwa kuendelea kutumia chombo hicho kuwajulisha Watanzania matukio mbalimbali yanayotokea hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Aidha, nawahakikishia wadau kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi mchango na kazi nzuri inayofanywa na redio hapa nchini ikiwemo kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uanzishaji wa redio nyingi zaidi.

Hadi Februari 12, 2020 jumla ya redio 204 zimesajiliwa hapa nchini ambapo redio 183 ni zile zinazorusha matangazo katika masafa ya redio na 21 ni redio za mtandao hali inayowafanya Watanzania kupata haki yao ya msingi ya Kikatiba.

Nawatakia wadau wote maadhimisho mema na sherehe za mwaka huu iwe chachu zaidi ya kuboresha vipindi na habari zinazotolewa na redio zetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...