WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
*Yawataka wahakikishe waliohamishwa mabondeni hawarudi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini wahakikishe wananchi waliokuwa wakiishi mabondeni ambao waliokolewa na kuhamishiwa kwenye maeneo salama hawarejei tena.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumatano, Januari 5, 2020) wakati akizungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha
Kipindimbi wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
“…haikubaliki
watu waliokuwa wakiishi mabondeni ambao kwa sasa wamehamishiwa kwenye
maeneo salama kuona wamerejea tena mabondeni. Wakuu wa Mikoa na Wilaya
hakikisheni wananchi hao hawarudi mabondeni.”
Waziri
Mkuu amesema Serikali inawataka wananchi hao kutorudi tena mabondeni
lengo likiwa ni kuwanusuru na maafa ya mafuriko yanayoweza kujirudia
kufuatia mvua kubwa zinazoendele kunyesha nchini.
Amesema
Serikali inawajibika kuhakikisha kwamba wananchi wote wanakuwa salama,
hivyo ni vyema kuchuwa hatua za kuwaondoa wote waishio mabondeni ili
kuwaepusha na maafa yanayoweza kuwapata.
Mbali
na kuzungumza na wananchi katika Kijiji hicho cha Kipindimbi, pia
Waziri Mkuu ametembelea vijiji vingine vilivyokumbwa na maafa hayo
ambavyo ni Nambilanje (Ruangwa), Nakiu na Njinjo (Kilwa) na Kitomanga
(Lindi) ili kujionea athari za mafuriko na kuwapa pole wananchi.
"Naomba
mpokee salamu za pole ninazozileta kwenu kutoka kwa Rais wetu mpendwa,
Dkt. John Pombe Magufuli alizozitoa kwa wananchi wote waliokumbwa na
mafuriko hayo kwa kupoteza ndugu zetu wapendwa pamoja na mali."
Awali,Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mvua hizo zilizonyesha
mfululizo zilisababisha maafa makubwa ambapo watu 21 walifariki huku
wengine 26,481 katika kaya 4,344 wakikosa makazi.
Bw.
Zambi alisema kuwa mbali na kusababisha vifo pia maeneo mbalimbali ya
kutolea huduma nayo yameathirika. Maeneo hayo ni pamoja na shule,
zahanati, miundombinu ya barabara, maji na mashamba ambayo yamefunikwa
na maji.
“Mvua
hizi zilisambaa katika wilaya zote za Mkoa wa Lindi, hata hivyo athari
kubwa zilitokea kwenye wilaya za Kilwa kata zilizoathirika ni saba,
Ruangwa kata 18, Liwale kata tatu na Lindi kata nne.”
Mkuu
huyo wa mkoa alisema mkoa wa Lindi ulikumbwa na maafa ya mafuriko
yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha Januari 18 na 19 na
ziliongezeka zaidi Januari 23 hadi 29, 2020.
Alisema
kutokana na nyumba nyingi kuzingirwa na maji au kubomoka shughuli za
uokoaji zilifanyika katika maeneo hayo ambapo watu waliookolewa
walihifadhiwa katika kambi za muda za uokoaji zilizofunguliwa katika
maeneo mbalimbali.
Alisema
mkoa umepokea misaada mbalimbali ikiwemo ya kutoka kwenye Ofisi ya
Waziri Mkuu kupitia Idara ya Mafaa ambayo imetoa mahema 80, mablanketi
50, ndoo 1,500, mikeka 350 pamoja na vikombe 350. “Pia tumepokea misaada
ya vyakula, nguo, dawa na vifaa vya shule kutoka kwa wadau
mbalimbali.”
Mkuu
huyo wa mkoa aliongeza kuwa walipokea vifaa vya uokoaji zikiwemo boti
nane kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), TFS, Halmashauri na
watu binafsi, Helikopta mbili kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi na mitumbwi
saba kutoka kwa watu binafsi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...