Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,  Meya wa jiji la Dar es Salaam Abdallah Mtinika, Balozi wa Jamhuri ya Uturuki nchini, Mhe.Ali Dovutoglu na Viongozi wa shule Turkiy Maarif Vakfi wakikata utepe kuzindua shule Turkiy Maarif Vakfi ambayo ni ya Taasisi ya Turkiy Maarif iliyopo Boko jijini Dar es Salaam leo.

WATURUKI hapa nchini katika kuunga mkono juhudi za Raidi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli, wawekeza kwenye Elimu kwa kuzindua shule ya Turkiy Maarif Vakfi iliyopo Boko jijini Dar es Salaam iliyopo chini ya Taasisi ya Turkiy Maarif  ya nchini Uturuki.

Akizngumza katika uzinduzi wa shule Turkiy Maarif Vakfi, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amesema kuwa shule hiyo iliyoanzishwa katika eneo la Boko jijini Dar es Salaam ni msaada mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu.

"Rafiki zetu nchi ya uturuki tunawapongeza sana taasisi ya Turkey Maarif  kwa kuchangia maendeleo ya nchi yetu". Amesema Prof. Ndalichako.

Tunafahamu kwamba serikali ya Awamu ya Tano kipaumbele chake ni Elimu ndio maana tunaona elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari.

Amesema matunda ya Elimu bila malipo yameshaanza kuoneka kama tunavyoona ongezeko la wanafunzi wa shule za awali za msingi na shule za sekondari pamoja na elimu ya awali. Hata hivyo amesema kuwa uhitaji wa shule umeongezeka kutokana na msongamano wa wanafunzi katika vyumba vya madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi.


"Tunawakaribisha wawekezaji katika kuwekeza katika sekta ya elimu kwa sababu mahitaji ya shule na mahitaji ya madarasa na mahitaji ya shule bado ni changamoto."

"Tunayo furaha sana kuwapokea ndugu zetu, rafiki zetu kutoka Uturuki kutoka taasisi ya Turkey Maarif Foundation ambao wamewekeza katika elimu. Amesema Dkt. Ndalichako.

Licha ya hilo Ndalichako amesema kuwa huu ni mwanzo tuu anawakaribisha kuwekeza makao makuu ya nchi Dodoma kuwekeza katika Elimu kwani wafanyakazi wengi wa serikali wanakaa Dodoma.


Kwa upande wa mkurugenzi wa shule ya Turkey Maarif, Aziz amesema kuwa katika uwekezaji katika elimu kwa sasa wanampango wa kuzindua shule nyingine jijini Arusha.
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa shule ya  Turkiy Maarif Vakfi  iliyopo chini ya Taasisi ya  Turkiy Maarif  iliyo nchini Uturuki, shule hiyo ipo Boko jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Uturuki nchini akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule ya Turkiy Maarif Vakfi iliyopo Boko jijini Dar es Salaam.

Meya wa jiji la Dar es Salaam Abdallah Mtinika akizungumza wakati wa kuzinduzindua shule ya Turkiy Maarif Vakfi iliyopo Boko jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu waliokuwepo kataka uzinduzi wa Turkiy Maarif Vakfi iliyopo Boko jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja.
Baadhi ya viti ambavyo vipo katika shule ya Turkiy Maarif Vakfi iliyopo Boko jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,  Meya wa jiji la Dar es Salaam Abdallah Mtinika, Balozi wa Jamhuri ya Uturuki nchini, Ali Dovutoglu na Viongozi wa shule Turkiy Maarif Vakfi wakibadilishana mawazo mara baada ya kuzindua shule ya shule Turkiy Maarif Vakfi ambayo ni ya Taasisi ya Turkiy Maarif iliyopo Boko jijini Dar es Salaam leo.

Wamasai wakitoa burundani katika uzinduzi wa shule ya Turkiy Maarif Vakfi iliyopo Boko jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...