Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SIMBA raha sana! Nidvyo unavyoweza kuzungumzia baada ya timu yao kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar  ya mjini Morogoro na kuifanya sasa kufikisha alama 53 , hivyo kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo kati ya Simba na Mtibwa umechezwa leo Februari 11 mwaka 2020 katika Uwanja wa Jamuhuri uliopo Mjii Morogoro, mashabiki walijitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo uliokuwa na fundi wa kila aina.

Mabao ya Simba yalifungwa na Nahodha wao John Bocco, Mohammed Hussein na bao la tatu lilifungwa na Hassan Dilunga.Ushindi wa Simba umerejesha matumaini ya timu hiyo kufanya vizuri.

Simba waliingia uwanjani wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi JKT Tanzania walioshinda mabao 1-0. Hivyo kuhakikisha katika mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa wanaibuka na ushinda na kupata alama tatu muhimu.Hivyo hadi dakika 90 za mchezo huo Simba wameibuka na ushindi huo.

Kikosi cha Simba kilichoibuka na ushindi huo, mlinda mlango ni Aishi Salum Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Tairone Santos, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Medie Kagere na John Bocco.

Hata hivyo Simba walionekana tangu mwanzo wa mchezo kulisakama lango la Mtibwa, hata hivyo umahiri wa walinzi wa Mtibwa pamoja na mlinda mlango wao ulisaidia kudhibiti mpira kuingia langoni.Kadri muda ulivyosonga ndivyo Simba ilivyokuwa ikitafuta nafasi zaidi na ndipo wakafanikiwa kuibuka na ushindi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...