Na Said Mwishehe,michuzi blog ya jamii.

WAZIRI Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye leo Februari 10 mwaka 2020 ametangaza  kurejea tena Chama Cha Mapinduzi (CCM)baada ya kuwa upinzani kwa miaka minne.

Sumaye aliihama  CCM ) wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ambapo alijiunga na CHADEMA ambacho kilikuwa miongoni mwa vyama vinne vya siasa nchini vilivyokuwa vinaunda Umoja wa Katika ya Wananchi( UKAWA) ambapo lengo ilikuwa kuing'oa CCM madarakani.

Mbali ya Sumaye mwingine aliyeondoka CCM katika mwaka huo wa uchaguzi mkuu alikuwa Waziri mstaafu Edward Lowassa ambaye naye alijiunga Chadema na kisha kupewa fursa ya kuomba Rais mwaka 2015, hata hivyo hakufanikiwa kushinda kiti hicho cha urais kwani Chama cha Mapinduzi kupitia mgombea wake Dk. John Magufuli awaliibuka na ushindi wa kishindo Lowassa tayari alisharejea CCM na kueleza kuwa yeye CCM ni nyumbani.

Akizungumza  leo ijini Dar es Salaam mbele ya katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashir Ally na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula   Sumaye amesema ameamua kurejea CCM ili apate fursa nzuri ya kuendelea kutoa ushauri kwa Taifa lake.

 Amesema kuwa  ametafakari na kuona ana kila sababu ya kurejea katika Chama hicho  ambacho kimemlea na kumkuza tangu akiwa mdogo,  hivyo amerejea ili ashiriki kikamilifu katika kushauri kwa kufuata utaratibu akiwa ndani ya Chama hicho.

"Nimeamua kurudi ili nitoe ushauri ndani ya Chama kwani kutoa ushauri nje ya Chama hakuna nguvu kwani unaonekana kama hauna maana hivyo nimerudi kwenye Chama changu tushirikiane kwa pamoja kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu."amesema Sumaye.

Amesema kwa niaba ya wanachama wote wa CCM nchini amewaomba wampokee  na kwamba yeye ni mwana siasa na ameifanya kazi hiyo kwa miaka mingi Sana hivyo atakuwa hatendi haki Kama atakaa tu mahali na pasipo kutoa mchango wowote kwa nchi yake.

" Sina hadhi  ya kudharaulika ndio maana nimeamua kurudi CCM ili hata ninapotaka kushauri basi nitumie Chama changu badala ya kuwa tu nashauri mtaani ambako hakuna naweza kuonekana sina heshima na nikadharaulika na nikashusha heshima yangu  "amesisitiza  Sumaye..

Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangulla akizungumza baada ya Sumaye kurejea CCM amesema inaeleweka kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi lakini ieleweke waliochaguliwa mwaka 2015 bado wapo kwenye nafasi zao.

"Rais wetu bado yupo kwenye nafasi yake, Diwani na Mbunge nap wapo kwenye nafasi zao hivyo yeyote anayekwenda kwenye Kata au Jimbo ajue anaofanya kosa la kimaadili  hivyo waliopo waachiwe watekeleze majukumu yao mpaka wakati uyakapofika na hiyo ni baadaya Bunge kuvunjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...