OFISI ya Rais TAMISEMI imejidhihirisha kwamba ni Ofisi ya wananchi kwa kuamua kufanya mambo magumu ambayo kwa jicho la kawaida unaweza kusema hayawezekani.

Hii imejidhirisha baada ya Waziri anayeongoza wizara hiyo kuwapongeza watu wake kwa kufanikisha ujenzi wa majengo mawili ya Kisasa katika Mji wa Serikali.

Majengo hayo ni jengo la Ofisi kuu ya TAMISEMI  na jengo la Makao Makuu ya TARURA.

Majengo hayo ambayo yamejengwa kwa maelekezo na usimamizi wa Waziri Jafo yamekuwa ni kivutio kikubwa katika Mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

Wizara hiyo imekamilisha majengo hayo ambayo yamejengwa kwa mtindo wa Ki-TAMISEMI yaani "Force Account" ni fundisho kwa Mikoa, Wilaya, na halmashauri zote nchini juu ya umuhimu wa kujali thamani ya fedha(value for money).
 Jengo la Ofisi Kuu ya Wizara ya Tamisemi kama linavyoonekana baada ya kukamilika.
Jengo la Ofisi Kuu ya Wizara ya Tamisemi upande wa nyuma linavyoonekana baada ya kukamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...