Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
hirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limempongeza Mjumbe wa Shirikisho hilo na Mjumbe wa Kudumu wa Yanga Dkt Tobias Lingalangala kwa kutunukiwa shahada ya uzamivu   (PHD- Doctorate in Humanity) mwishoni mwa wiki hii.

Lingalangala ametunukiwa kutoka Chuo cga LeadImpact cha Nchini Marekani baada ya kuonesha mchango wake mkubwa kwa jamii.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TFF,Makamu wa Rais Stephen Mguto amesema wamefurahi sana kuona moja ya mdau wakubwa wa mpira wa miguu kutunukiwa shahada ya uzamivu kutoka chuo cha LeadImpact.

Mguto amesema, wameamua kumpa zawadi kama motisha kwake kutokana na mchango wake mkubwa kwa jamii na mambo ya mpira.

"TFF imeona mchango mkubwa unaofanywa na Lingangala na sisi hatukutaka kuona linapita na ndio maana tumemuita hapa aje tumpatie zawadi," amesema.

Naye Lingalangala amesema hakuwa akitarajia kupokea simu ya Rais wa TFF Walace Karia mapema leo akimtaka afike ofisi za Shirikisho ili kumpongeza na kumpa zawadi.

Anashukuru kwa kwa zawadi aliyoipata kutoka Shirikisho, na kwakuwa wameona mchango wake mkubwa kwa Jamii na hata mpira.

"Sikutegemea kama shahada yangu hii (PHD) ingekuwa na umuhimu mkubwa kwa watu wangu wa karibu na leo nimepigiwa simu na Rais Karia akinipongeza na kutaka nifike hapa ofisini kukabidhiwa zawadi zangu," amesema Lingalangala.

Mbali na hilo, Lingalangala amekuwa na mchango mkubwa sana kwa mpira wa Tanzania kwa muda mrefu ambapo kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF wanaowakilisha Mkoa wa Njombe.

Lingalangala amekabidhiwa shahada ya uzamivu baada ya Chuo cha Lead Impact kuona mchango wake mkubwa katika jamii ikiwemo Kilimo na ufugaji wa kisasa na Miradi ya maendeleo aliyoijenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...