Dodoma,
09 Februari, 2020
Waziri
wa Kilimo Mhe.Japhet N.Hasunga (Mb) leo Jumapili anawafahamisha wakulima na
wananchi kwa ujumla kuwa taarifa zinazoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari
na mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa nzige wa Jangwani nchini hususan mkoa wa Kilimanjaro siyo za kweli.
Mhe.Hasunga
amesema hayo wakati alipoongea na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1) na
kusema “ hakuna taarifa za kitaalam
zilizothibitisha uwepo wa nzige kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ila ni
kweli Kuna nzige wameonekana Kaunti ya Kajiado nchini Kenya takribani kilomita
50 toka mpakani na Tanzania” alisema
Waziri wa Kilimo
Wataalam
wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo duniani
(FAO) linaendelea na ufuatiliaji wa viashiria vya uwepo wa nzige na tayari
hatua za awali za kuwadhibiti endapo wataingia nchini zimechukuliwa. Hatua hizo
ni pamoja na Mashirika ya kimataifa ambayo sisi ni wanachama kutuahidi ndege
tatu maalum za kunyunyizia dawa na uwepo wa dawa za tahadhali kwenye mikoa ya
Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Wizara
inatoa wito kwa wakulima, maafisa ugani na kilimo na wadau wote wa kilimo
kuendelea kutoa ushirikiano wa taarifa sahihi kwa serikali endapo kutajitokeza
viashiria vya nzige kwenye maeneo ya mashamba.
Aidha,vyombo
vya habari vinasisitizwa kutoa taarifa sahihi na za ukweli ili kuepusha
sintofahamu kwa wakulima.
Imetolewa
na ;
Prof. Siza D. Tumbo
KAIMU
KATIBU MKUU



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...