Addis Ababa, Ethiopia,
Tanzania
imeunga mkono wazo la kutaka nchi za Kiafrika kuwa na vyanzo mbadala
vya fedha ili kukabiliana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia
nchi na kutoa wito kwa nchi zilizoahidi kuchangia fedha za kukabiliana
na mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano wa Paris kuheshimu ahadi zao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameyasema hayo katika mkutano wa 33 wa wakuu wa nchi na serikali wa
Umoja wa Afrika unaoendelea Addis Ababa, Ethiopia wakati wa mjadala
kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na njia za kukabiliana na
athari zake na kuzisihi nchi zilizoahidi kutoa michango katika mkutano
wa Paris kuhusu mazingira kuheshimu ahadi zao.
Mhe
Samia Suluhu Hassani ameongeza kuwa kutokana na athari za mabadiliko ya
tabia nchi kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma jitihada za maendeleo ya
nchi za Afrika kutokana na uharibifu wa miundo mbinu pia vifo
vinavyotokana na vimbunga,mafuriko ama ukame unaosababishwa na
mabadiliko ya tabia nchi na kuunga mkono wazo la Nchi za Afrika kuwa na
mfuko maalum pamoja na vyanzo mbadala vya kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi.
Suala
la elimu nalo lilipata fursa ya kujadiliwa katika mkutano huu wa 33 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika ambapo Tanzania imepata
nafasi ya kuchangia mjadala huo na kuridhia wito wa kuzitaka nchi zote
za Afrika kuongeza bajeti zake katika sekta ya elimu ili kuwawezesha
vijana wa kiafrika kupata elimu iliyo bora nay a ushindani.
Taarifa
ya mpango wa Nchi za Afrika kujitathmini kiutawala bora
yaani APRM,iliyowasilishwa na Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika ambaye
pia ni Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa ameitaja Zimbabwe
kuwa ni mojawapo ya nchi ambazo zimeridhia na kusaini mpango huo jambo
ambalo Tanzania kupitia kwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
ameipongeza Zimbabwe licha ya hali mbaya iliyonayo na mapito inayopitia
ikiwa ni pamoja na vikwazo vya kimataifa.
Mkutano
huo wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika umeingia
katika siku yake ya pili ukitanguliwa na ule wa Baraza la Mawaziri wa
Umoja huo uliofanyika kuanzia Februari 6 hadi 7 mjini Addis Ababa Nchini
Ethiopia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...