Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara katika serikali ya Awamu ya Tatu Mzee Iddi Mohamed Simba amefariki dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, binti yake Sauda Simba amethibitisha.

RATIBA YA MAZISHI
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mwili wa Marehemu Iddi Mohamed Simba utaoshwa katika msikiti wa Maamur ulioko Upanga jijini Dar es salaam kabla ya kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni Plot 109 mnamo saa mbili asubuhi, ambapo ndugu, jamaa, marafiki na majirani watakusanyika kumuombea  dua hapo nyumbani.

Itapofika saa 5 asubuhi mwili wa Marehemu utapelekwa msikiti wa Manyema mtaa wa Mafia na Lumumba, Kariakoo,  ambapo kutakuwa na dua pia. Kisha baada ya swala ya Ijumaa, itafuatia Swalat Jeneiza kisha mwili utapelekwa Magomeni kwenya makaburi ya Mwinyimkuu kwa mazishi.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un 
إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...