Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na mameneja (hawapo pichani) wakati wa kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Kulia ni meneja wa TEMESA mkoa wa Arusha Mhandisi Heriel Mteri na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Vivuko Mhandisi Adelard Kweka.
Mameneja wa mikoa na vituo wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Maselle (katikati) mara baada ya kumaliza kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Meneja wa Uchumi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Frederick Gwanchele akisoma taarifa kwa mameneja wa vituo na mikoa wa Wakala huo wakati wa kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Baadhi ya mameneja wa mikoa na vituo wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA waliohudhuria kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 wakisikiliza kwa umakini taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.PICHA ZOTE NA TEMESA (ARUSHA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...