Makamu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Momole Kasambala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo ya wajasiriamali Manispaa ya Temeke yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo yaliyofanyika katika Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa TIA Fedha na Utawala wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt.Matei Mapunda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo kwa wajasiriamali namna watavyoweza kuendesha biashara kutokana na mafunzo hayo yaliyofanyika katika Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam
Mratibu wa Mafunzo Mafupi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Dkt Isaya Hasanali akitoa maelezo kuhusiana namna watavyoendesha mafunzo kwa wajasiriamali ,mafunzo hayo yalifanyika katika Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Lilian Mpanju akizungumza kuhusiana mafunzo kwa wajasiriamali yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo
Mjasiriamali Abbakari Milazi akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo yatavyowasaidia katika kuendesha biashara zao
picha ya pamoja ya watendaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na wajasiriamali wa manispaa ya Temeke



*Mafunzo ni endelevu kuwawezesha kusimama katika biashara

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imesema kuwa wajasiriamali wadogo wadogo wanaendesha biashara bila kuwa na misingi mafunzo maalumu ya kuendesha biashara hizo.

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo kwa wajasiriamali kushindwa kusimama na biashara zao Taasisi ya Uhasibu nchini imekuja na program ya mafunzo kwa wajasirimali kuwafundisha namna ya kuendesha ujasiriamali kitaalam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya Wajasiriamali Manispaa ya Temeke Makamu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Momole Kasambala amesema kuwa wameanza na Manispaa ya Temeke na baadae wataanza kwenda sehemu nyingine kutoa mafunzo ya uendeshaji wa biashara kwa wajasiriamali.

Amesema wajasiriamali wanajituma katika kufanya biashara lakini wanakosa elimu ya kufanya biashara zao ziweze kukua hivyo kwa mafunzo hayo yatawaongeza ujuzi wa kusimamia biashara wanazozifanya.

Dkt.Kasambala amesema kuwa Taasisi za Fedha zinakopesha wajasiriamali hivyo wanahitaji kujengewa uwezo jinsi ya kuendesha biashara na sio urejeshaji wa fedha wakati biashara haziendi vizuri.

Nae Makamu Mkuu wa TIA Fedha na Utawala Dkt.Matei Mapunda amesema kuwa wajasiriamali wanatakiwa kwenda na kasi kutokana na serikali kwenda katika uchumi wa kati hivyo wajasiriamali wanatakiwa ndio kuwa wa kwanza kuwekeza viwanda vidogo.

Amesema kuwa wajasiriamali wanahitaji kutangaza biashara ili ziweze kukua na sio kufungia na kuuza biashara kwa jamii moja wakati wanaweza kuuza ndani na nje ya nchi.

Mjasiriamali Abbakari Milazi amesema mafinzo wanayopata yatawasaidia katika uendeshaji wa biashara kwani wanaendesha biashara kienyeji.Amesema TIA imethubutu kujitolea mafunzo kwa wajasiriamali kwani taasisi chache ambazo zinaweza kugharamia mafunzo bila malipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...