Na Karama Kenyunko globu ya jamii.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania nchini, (TMA) imesema katika siku tatu zijazo itanyesha mvua kwa baadhi ya maeneo machache ya pwani ya kaskazini ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kumalizika kwa kipindi cha hali ya joto kuwa juu ya wastani kutokana na kuwepo kwa jua la Utosi katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu.
Siku tatu zilizopita yaani Februari 9-11 mwaka huu hali ya joto nchini hususani katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Morogoro na Tanga ilikuwa na joto kali sana hali mpaka kufikia wastani wa kupelekea shida kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya siku moja iliyofanyika katika ofisi za TMA zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt.Agnes Kijazi amesema mvua zitakazonyesha zitafanya hali ya joto kuzidi kushuka ambapo zitaanza Februari 12 hadi 14 mwaka huu.
Dkt.Kijazi amesema hali hiyo ya joto sio endelevu kwani joto linapokuwa jingi linatengeneza unyevunyevu angani na kutengeneza vipindi vya mvua.
"Kwa siku hizo mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na joto kuanzia nyuzi jonato 33.3 mpaka 33.9 na wastani wake ukiwa ni nyuzijoto 32.6 huku kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro nyuzi joto ikifikia nyuzi joto 34.2 huku
mkoa wa Tanga ulikuwa na nyuzijoto ipo juu na kufikia 36," amesema
Alisema hali hiyo ya joto sio ya kudumu na kwa leo (jana) hali imebadilika na kufanya joto kupoa na kuanzap kunyesha kwa mvua ambapo zitanyesha siku tatu mfurulizo.
Aidha kesho Februari 13,2020 TMA itatoa utabiri wa mvua za masika (MAM) zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni kwa baadhi ya maeneo ya mikoa mbalimbali.
Dkt.Kijazi amesema Warsha hiyo ni muendelezo wa juhudi za mamlaka kutaka kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa ikiwemo jamii kwa uhakika, usahihi na kwa wakati.
Amesema tqarifa za hali ya hewa zikiifikia jamii kwa wakati, zitaisaidia jamii kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa pia itazisaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango endelevu ambayo haiwezi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa na kuuzia madhara mbali mbali ikiwemo vifo na mafuriko.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akifafanua jambowakati akifungua semina ya waandishi wa habari leo katika makao mkuu ya taasisi hiyo kuhusu utabiri wa hali ya Mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2020 kushoto ni Dk. Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA na kulia ni Willbeforce kikwasi Kaimu Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akimsikiliza Dk Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA wakati akizungumza katika semina hiyo.
Mchambuzi wa hali ya hewa Abubakar Lungo akielezea jambo wakati akizungumzia rasimu ya utabiri wa Mwelekeo wa hali ya Hewa Msimu wa Mvua za Masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2020.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...