MAMLAKA ya hali ya hewa nchini (TMA) imetoa mwelekeo na hali ya mvua za masika kwa mwezi Machi hadi Mei 2020 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua huku akitoa angalizo kwa wananchi kufuatilia utabiri unaotolewa na mamlaka hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 13 2020 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,  Dkt. Agnes Kijazi amesema kuwa mvua za wastani  hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka na kueleza kuwa maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini mashariki yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Dkt. Kijazi amesema kuwa mvua za masika ni mahususi katika maeneo ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki, Pwani ya Kaskazini na visiwa vya Unguja na Pemba, Ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini wa Mkoa wa Kigoma na sehemu kubwa ya maeneo hayo yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani katika msimu wa masika kwa mwaka 2020  na katika baadhi ya maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki hasa katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro uwezekano wa wa kunyesha kwa mvua za juu ya wastani ni mkubwa.

Akifafanua hali ya kunyesha kwa mvua hizo Dkt.Kijazi amesema kuwa kwa maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria kwa Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita,Simiyu na Shinyanga mvua kwa maeneo hayo zinatarajiwa kuwa wastani hadi chini ya wastani na zinatarijwa kuanza kunyesha katika wiki ya pili ya  mwezi Machi na kumalizika  katika wiki ya tatu ya mwezi Mei ambazo zinatarajiwa katika mikoa ya Kagera Magharibi mwa Mkoa wa Geita na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma Wilaya za Kakonko na Kibondo.

Maeneo ya ukanda wa Pwani ya kaskazini mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba  mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani hiyo ikijukuisha pamoja na visiwa cha Mafia ambapo mvua katika maeneo hayo zinatarajiwa kuanza kunyesha kati ha wiki yankwanza na ya pili ya mwezi Machi na kumalizika wiki ya tatu ya mwezi Mei 2020.

Katika maeneo ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki, mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi na hivyo wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari.

Aidha TMA imetoa angalizo la kuwepo uwezekani wa kutoka vipindi vifupi vya ukavu katika wiki ya kwanza ya mwezi Mei na mvua kubwa unaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.


Wakati huo huo mamlaka hiyo imetoa tahadhari na ushauri kwa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, mifugo, nishati na madini, mamlaka za maji, sekta za afya, menejimenti ya maafa na vyombo vya habari kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua za masika  ikiwa ni pamoja na kupata na kufuata ushauri wa wataalamu wa mamlaka hiyo kwa kuzingatia mvua hizi zitanyesha kwa muda mfupi, na pia amewataka wananchi kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamalaka hiyo kila wakati na kusisitiza kuwa Mamlaka ya hali ya hewa nchini itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi wa kwanza kulia  akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa utabiri b wa mvua za masika katika kipindi cha Machi hadi Mei mwaka 2020. Katikati ni Dk Hamza Kabelwa MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA na mwisho ni Rose Senyagwa mtaalam wa hali ya hewa.
 Mtaalamu wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA, Rose Senyangwa akichambua Utabiri wa hali ya hewa wakati wakisoma Utabiri wa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza kunyesha mwezi Machi hadi Mei mwaka 2020. Aliyeko katikati ni dk. Hamza Kabelwa Mkurugenzi wa huduma za utabiri na kulia ni Mkurugenzi wa TMA dkt Agnes Kijazi

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...