Katika picha ya pamoja, Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania, BI. Devota Mdachi (Kushoto) akiwa na mrembo
Graatness Nkuba pamoja na Meneja wake Miriam Ikoa.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
imeendelea kutumia fursa ya mashindano ya urembo ya kimataifa
kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi Devota Mdachi amemkabidhi mrembo
Graatness Nkuba bendera na vipeperushi vyenye taarifa za utalii wa
Tanzania kabla ya kuanza safari yake ya kwenda kushiriki shindano la
urembo nchini Vietmnam.
Mlimbwende Greatness ni
Mtanzania pekee anayetarajia kuiwakilisha Tanzania katika shindano la
“Miss Charm International” ambalo linalenga kumtafuta mrembo mwenye
haiba, mvuto na ambaye atabeba utamaduni, elimu na kuutangaza utalii wa
nchi yake. Shindano hili litahusisha warembo kutoka nchi 50, linatarajia
kufanyika katika mji wa Ho Chi Minh nchini Vietman kuanzia tarehe 5 –
17 mwezi machi, 2020.

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania, BI. Devota Mdachi akimkabidhi bendera mrembo Graatness A.
Nkuba katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam.

Mrembo Graatness Nkuba akionyesha baadhi ya vipeperushi akivykabidhiwa na Bodi ya Utalii Tanzania.
……………………………………………………………………………………………………..
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
imeendelea kutumia fursa ya mashindano ya urembo ya kimataifa
kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi Devota Mdachi amemkabidhi mrembo
Graatness Nkuba bendera na vipeperushi vyenye taarifa za utalii wa
Tanzania kabla ya kuanza safari yake ya kwenda kushiriki shindano la
urembo nchini Vietmnam.
Mlimbwende Greatness ni
Mtanzania pekee anayetarajia kuiwakilisha Tanzania katika shindano la
“Miss Charm International” ambalo linalenga kumtafuta mrembo mwenye
haiba, mvuto na ambaye atabeba utamaduni, elimu na kuutangaza utalii wa
nchi yake. Shindano hili litahusisha warembo kutoka nchi 50, linatarajia
kufanyika katika mji wa Ho Chi Minh nchini Vietman kuanzia tarehe 5 –
17 mwezi machi, 2020.
Akiongea wakati wa hafla ya
makabidhiano yaliyofanyika Februari 21, 2020 katika ofisi ya TTB iliyopo
jijini Dar es salaam, Bi. Devota alisema “Tunakukabidhi vipeperushi
ambavyo ni nyezo utakayoitumia kuwahamasisha na kuwavutia warembo
wengine waje kuvitembelea na kujionea utajiri wa vivutio vya asili
vilivyopo katika nchi ya Tanzania pamoja na kuipeperusha bendera ya
Tanzania katika mashindano hayo ili dunia itambuwe kuwa “Tanzania
Unforgettable”.
Tanzania kuwa na mwakilishi katika mashindano haya kutasaidia kulifungua soko la utalii la nchi ya Vietnam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...