Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Katika kuendeleza juhudi za kutunza Ziwa Victoria ubalozi wa Ufaransa hapa nchini umeendesha mdahalo wa ulioshirikisha wadau mbali mbali wakiwemo watafiti wa uvuvi.
Akizungumza katika mdahalo uliofanyika Alliance France jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Ishmael Kimirei ameseema njia za kutunza Ziwa Victoria ni kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali ambazo zinapaswa kuchukuliwa hatua ikiwemo kuondoa kemikali za Viwandani zinazoingia Ziwani na kuepuka kilimo cha kutumia kemikali pembezoni mwa Ziwa.
Amesema, mabadailiko ya tabia nchi pia ni moja wapo ya changamoto inayosababusha ugumu katika kutunza ziwa hilo lakini yapo mambo magumu zaidi kuliko hayo ambayo yanahitaji utaalamu mkubwa kutatua ikiwemo uwepo wa magugu maji, uvuvi haramu na uchafuzi wa mazingira.
Amesema kazi ya kuondoa uvuvi haramu iliyofanywa mwaka jana mwezi wa tisa, kupitia doria nyingi zilizofanywa na serikali kwa ushirikiano na Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweza kusimamia tatizo la uvuvi haramu mpaka kupatikana faida ya kuwepo kwa samaki mara dufu.
Amesema katika utafiti waliofanya hivi karibuni katika maziwa likiwemo Ziwa Victoria na bahari Kuu kuangalia msingi wa samaki unaonyesha uwingi wa samaki umeongezeka mara dufu tangu baada ya kuanza kwa zoezi hillo la kuondoa uvuvi haramu.
"Bado kuna watu wanafanya uvuvi haramu, tunawaasa waache kufanya hivyo mara moja kwa sababu Ziwa Victoria ni mali ya kila mtanzania, resources ya samaki ni mali yetu sote, viwanda haviwezi kupata Samaki kutoka kule kama uvuvi haramu utaendelea",
amesema
Pia ameongeza kuwa uchafuzi wa mazingira ni moja ya vitu vinavyochangia uharibufu katika Ziwa Victoria. Kwani
Kuna utiririshaji wa maji machafu kutoka viwandani, mtiririsho wa maji yenye mbolea nyingi za kisasa kutoka mashambani na kuwapo kwa matumizi yasiyoendelevu ya ardhi, yaani inatokea kwamba udongo unaozalishwa mashambani kwa kukata miti, yote inaingia kwenye ziwa victoria.
Amesema, udongo unapoongezeka Ziwani unasababisha tope na hivyo kusababisha kina cha maji kupungua.
‘’Ziwa letu linaathiriwa na matumizi yetu binadamu, lakini mabadiliko ya tabia ya nchi, kwa upande wa shughuli za binadamu ni pamoja na matumizi ya kemikali kwenye kilimo katika maeneo ya karibu na ziwa, kinachosababisha samaki kuathirika. Lakini udongo unaotoka shambani na kuingia ziwani unapelekea kupunguza kina cha maji sasa njia ya kutunza ziwa letu ni kuhakikisha tunaondoa haya yote,’’ amesema Kimirei.
Kwa upande wake, Balozi wa Ufaransa nchini, Fredrick Clavieter amesema Ufaransa inathamini urithi w8a kizazi kijacho cha watanzania na kuona kuwa kuna umuhimu wa kupunguza matumizi ya kemikali viwandani na kwenye kilimo ambazo zinaingia kwenye ziwa na kuathiri ziwa hilo.
Ili kufanikisha hilo, Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha usalama wa Ziwa Viktoria na kuendelea kutafuta namna bora ya kutunza ziwa hilo.
Aidha, ameongeza kuwa ufaransa kupitia shirika lake la msaada, limeweka kiasi cha USD milioni Moja kwa ajili ya kilimo cha asili kisichotumia kemikali ili kudhibiti uchafuzi unaotokana na shughuli za kilimo na kuishia ziwani.
Msaada huo utawasaidia wakulima wadogo 8000 kuwa na mbinu za ubunifu ambazo haziharibu mazingira na kwamba suala la uhifadhi wa mazingira ni kipaumbele cha serikali ya Ufaransa, Rais Emmanuel Macron ameonyesha uthabiti katika kulinda viumbe hai na mazingira.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...