Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

UCHAGUZI wa urais nchini Malawi iliyofanyika Mei mwaka jana na Rais Peter Mutharika kushinda umefutiliwa mbali na mahakama ya kikatiba nchini humo na kuelezwa kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki moja ya chombo cha habari nchini humo kimeripoti.

Kupitia mtandao gazeti la Lake Nyasa limeripoti kuwa mahakama hiyo chini ya majaji watatu imeeleza kugundua makosa tele katika uchaguzi huo na hata taratibu za utangazaji matokeo hazikizingatiwa.

Imeelezwa kuwa mahakama hiyo imesema kuwa uchaguzi huo uliofanyika Mwezi Mei mwaka jana na Mutharika kushinda kwa asilimia 38 dhidi ya mpinzani wake Chakwera Lazarus aliyeshinda kwa asilimia 35 uligubikwa na udanganyifu na matokeo yake yalikuwa na makosa mengi.

Imeelezwa kuwa Televisheni ya taifa haikurusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika mahakama hiyo huku uchaguzi mpya wa maruduio ukielekezwa kufanyika ndani ya kipindi cha siku 150.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...