Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
UMOJA wa wajasiriamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa sabuni nchini, wamezindua rasmi umoja wao unaokwenda kwa jina la Umoja wa Watengenezaji Sabuni wadogo Tanzania (UWASWATA) utakaokuwa unafanya kazi chini ya mwavuli wa Shirika linalosimamia viwanda vidogo vidogo (SIDO) na ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali.
Akizungumza na blogu ya jamii mara baada ya kuzindua umoja huo katibu mkuu wa umoja huo Maria Lucas amesema kuwa umoja huo una malengo ya kuwainua wajasiriamali hao pamoja na kujenga viwanda vidogo kama Serikali ya awamu ya tano ilivyodhamiria.
"Hii ni fursa kwa wajasiriamali wa utengenezaji wadogo wa sabuni, kwa kuwa umoja huu utatusaidia sana katika kupata uthibitisho wa uanachama pamoja na kupata elimu ihusuyo kujikinga na kemikali ambayo ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali inaisimamia." Ameeleza.
Aidha amesema; kupitia umoja huo wanachama watapata fursa kuhusiana na uboreshaji wa bidhaa zao ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya chama hicho ya "Usafi Daima, Tanzania ya viwanda."
Vilevile Mwenyekiti wa umoja huo Patric Mbogela amewashauri wajasiriamali wa utengenezaji sabuni jijini Dar es Salaam kutumia fursa hiyo kwa kuwa wanachama wenye ithibati ili kutengeneza bidhaa yenye ubora na kuwa na sauti pamoja na nguvu moja katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
Aidha kwa upande wake mkufunzi na mlezi wa Chama hicho George Buchafwe amesema kuwa, kufuatia mkutano waliofanya na mkemia mkuu wa serikali na kujadili namna ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wa sabuni hasa kwa kuepukana na kemikali wanazotumia na kujisajili kwa mkemia mkuu wa serikali wakaona ni vyema kuwakutanisha wajasiriamali hao na kuunda umoja huo ambao utabeba sauti moja katika kuendeleza viwanda vidogo.
Amesema kuwa wamekutana na kuunda uongozi amWbao wanaamini watasimamia vyema na kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli iliweka mbele kipaumbele ujenzi wa viwanda.
Vilevile amewashauri wajasiriamali wadogo wa sabuni Dar es Salaam kutumia fursa kwa kutembelea ofizi za SIDO na kujiandikisha ili wawe sehemu ya umoja huo na kupata uthibitisho wa wanachama.
Katibu mkuu wa Chama cha umoja wa Watengenezaji wa sabuni Tanzania (UWASATA) Maria Lucas akizungumza mara baada ya kuzindua umoja huo ambapo ameeleza kuwa malengo na madhumuni ya umoja huo ni Kuhakikisha kila mwanachama anapata ithibati, manufaa na elimu ya kuzalisha bidhaa bora zaidi, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa umoja wa Watengenezaji Sabuni Tanzania (UWASWATA) Patric Mbogela akizungumza mara baada ya uzinduzi wa umoja huo na kuwashauri wajasiriamali kote nchini kutumia ofisi za SIDO ili kupata uthibitisho, leo jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi na mlezi wa umoja wa Watengenezaji Sabuni Tanzania (UWASWATA) George Buchafwe akitoa mafunzo kwa wajasiriamali hao na kuwashauri kuendelea kushirikiana hasa kwa kuboresha bidhaa zao na kutafuta masoko, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya bidhaa walizotengeneza, leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...