Baadhi ya picha zilizotumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika kitabu cha "A Taste of Tanzania." 


Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiteta jambo na mpiga picha aliyeshiriki katika maandalizi ya uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho, Bw. Wim Demessemaekers.
Mhe. Balozi kasanju akipokea ufafanuzi wa tafsiri za picha mbalimbali kutoka kwa Bw. Wim
Balozi wa Yemen nchini Uholanzi, Mhe. Sahar Ghanem akimsalimia na kumpongeza Bw. Wim kwa umahiri wake wa kupiga picha. Mhe. Ghanem alielezea nia yake ya dhati ya kutembelea Tanzania.
Sehemu ya Wanadiplomasia, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wadau wengine walioshiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa Kitabu na ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii wa Tanzania.
Baadhi ya vyakula vya kitanzania vilivyoandaliwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa kitabu na ufunguzi wa maonesho.



Dodoma, 5 Februari 2020

Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi umeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoitwa “A Taste of Tanzania” kilichosheheni picha zinazoonesha vivutio vya utalii pamoja na utamaduni wa Mtanzania. Uzinduzi wa Kitabu hicho chenye kurasa 343 ulifanyika wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii uliofanyika The Hague, Uholanzi tarehe 30 Januari 2020.

Maeneo ya utalii yanayooneshwa kwa kina ndani ya Kitabu hicho ni pamoja na; Mji wa kimataifa wa Arusha; Mlima Kilimanjaro; Hifadhi za Taifa za Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Tarangire na Ruaha; Mlima Ol Donyo Lengai na Ziwa Natron. Maeneo mengine ni Olduvai Gorge; umaarufu wa Ziwa Eyasi na Bonde la Ufa; Utalii wa mkoa wa Iringa; aina mbalimbali za mapishi pamoja na viungo vyenye ladha nzuri vinavyoleta upekee katika mapishi hayo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa sherehe ya Uzinduzi wa Kitabu na Maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju aliwashukuru waandaji wa Kitabu hicho kwa uwasilishaji sahihi kuhusu Tanzania, hali itakayowezesha watalii kuongezeka zaidi nchini, Balozi Kasyanju alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa Waholanzi na Jumuiya ya Kimataifa kuja kuwekeza Tanzania kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika katika miundombinu na taratibu za uwekezaji.

“A Taste of Tanzania” ni kitabu kilichoandaliwa na mwandishi Bw. Stephen Walckiers kwa kushirikiana na mpiga picha maarufu, Bw. Wim Demessemaekers, wote wakazi wa Uholanzi waliowahi pia kuishi Tanzania. Uzinduzi rasmi wa kitabu hicho kinachopatikana kwenye mitandao na maduka ya vitabu nchini unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania tarehe 05 Februari 2020.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...