

************************
Nteghenjwa Hosseah, Dar es salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) amewataka
vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa za mikopo ya vijana
inayotolewa katika kila Halmashauri Nchini.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati
alipokua akifungua Kampeni ya Vijana Twende inayolenga Vijana wa Dar es
salaam kuchangamkia fursa za kujukwamua kiuchumi iliyofanyika katika
ukumbi wa Ubungo Plaza, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika ufunguzi huo
Waziri Jafo amesema Kampeni ya Vijana Twende itasaidia kuhamasisha
vijana wa Mkoa wa Dar es alaam kuchangamkia fursa za kiuchumi
zinazotolewa na Serikali, ikiwemo mikopo ya vijana (4%) kutoka
halmashauri za jiji la Dar es salaam pamoja na zile zinazotolewa na
wadau wangine wa maendeleo.
« Msingi mkuu wa kampeni hii ni
kubadili fikra na tabia za vijana na kuwafanya vijana Kuwa na uwezo wa
kutengeneza makundi ya kuwazalishia kipato na Kuwa na vijana wenye
maadili ya kuchapa kazi,kutokutukutumia madawa ya kulevya, wasiowazembe,
wanaojali muda na wenye matumizi ya fedha yenye tija.
Aliongeza kuwa tunataka tupate
vijana walioungwa katika duru za maamuzi katika ngazi mbalimbali kuanzia
mtaa,kata,wilaya,mkoa na Vijana wanaoshiriki kikamilifu katika shughuli
za kijamii » alisema Jafo
Kwa Kampeni hii napenda kutambua
mchango wa Shirika la Baba Watoto Organisation kupitia Ufadhili wa
shirika la Foundation for Civil Society (FCS) ambao umewezesha kufanyika
kwa shughuli mbali mbali za mradi na vijana wengi kuhamasishwa na
kujengewa uwezo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kupunguza
tatizo la ajira na kiwango cha umaskini katika nchi yetu.
Alimalizia kwa kusema kuanzia sasa
sina mashaka na vijana wa Dar es salaam naamini kupitia Kampeni hii
watakua wamepata uelewa wa kutosha wa namna ya kupata mikopo inayotolewa
na Serikali na ile ya wadau.
Akizungumza katika Kampeni hiyo
Meneja Programu toka Foundation for Civil Society Francis Uhadi
amemuomba Waziri Jafo kuwa ikiwezekana idadi ya vijana wanaotakiwa
kujiunga katika makundi ili kuomba mikopo kwenye Halmashauri ipungue
kutoa vijana kumi hadi kufikia watano ili kurahisisha upatikanaji wa
vijana hao.
Aliongeza kuwa muda wa kuomba hadi
kupatiwa mikopo hiyo uwe mfupi kidogo kwani kwa sasa huwa inachukua
miezi sita hadi mwaka hivyo kuwakatisha tamaa waombaji.
Naye Mkurugenzi wa Baba Watoto
Organisation Oscar Kapande amesema shughuli za mradi wa Vijana Twende
zimetekelezwa katika Miji nane(8)ya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo
Mbeya, Dodoma, Mwanza, Arusha, Longido ,Unguja,Pemba na Dar es salaam.
Ameongeza kuwa haya ni maono muda
mrefu ya Shirika hilo ya kuhudumia vijana katika nyanja mbali mbali za
Maisha, pamoja na kuchukua hatua hii ya kuhamasisha na kujengea uwezo
vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...