Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeeleza kusikitishwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi na makundi ya kisiasa na kijamii zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora huku ikielezwa kuwa kauli hizo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa wananchi kujichukulia Sheria mikononi kutokana na kutoridhishwa na vitendo vya baadhi ya wanasiasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jaji mstaafu Mathew Mwaimu imeeleza kuwa, hivi karibuni kumekuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za vitisho dhidi ya wengine kutokana na kutofautiana kimtazamo, huku makundi mengine yamejitokeza kupinga hatua hiyo na kuahidi kuchukua hatua ambazo hazitoi sura nzuri katika Ustawi wa misingi ya haki za binadamu na utawala bora nchini jamii.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa tume hiyo inasisitiza umuhimu wa kuvumiliana na kutumia taratibu za kisheria katika kutafuta ufumbuzi wa masuala kadha wa kadha yanayolalamikiwa  kwa kuwa kauli hizo zisipodhibitiwa zinaweza kupelekea uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini.

Aidha kupitia taarifa hiyo imeelezwa kuwa;

"Tume inaviomba vyama vya siasa kusimamia na kuwadhibiti wafuasi wao kutotumia lugha ambazo zinaweza kupelekea uvunjivu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora" imeelezwa.

Aidha taarifa hiyo imesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kupinga kauli hizo na kudumisha amani na utulivu katika nchi yetu tunu ambayo imedumu kwa muda mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...