Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu Mkuu wa wizara
ya Elimu sayansi na teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo amevitaka vyuo ya
ualimu 35 nchini kuvituza vifaa na vitabu walivyopewa kutoka serikali ya
Canada ili kusaidia kuongeza ubora wa elimu nchini.
Dkt.Akwilapo
Aliyasema hayo wakati akikabidhi vifaa na vitabu vya kufundishia na
kujifundishia waalimu ikiwa ni sehemu ya mradi wa kuendeleza elimu ya
ualimu TESP wenye thamani ya zaidi ya bilion 90 kwenye hafla
iliyofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa msingi
na uboreshaji elimu nchini unaanzia kwenye ufundishaji wa wanafunzi
hivyo fedha na vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kwa lengo kuu la
kuboresha elimu.
Akaeleza kuwa lengo
kuu la mradi huo wa kuendeleza elimu ya ualimu ni kuboresha mazingira
ya ufundishaji na ujifunzaji kwa waalimu nchini ili kukuza viwango vya
elimu zao kwenye ufundishaji wanafunzi nchini.
“Ni mategemeo ya
serikali kuona vifaa hivi vikituzwa kuweza kusaidia vizazi vijavyo
kuhakikisha uboreshaji wa elimu nchini huku akiwataka wakuu wa vyuo
kuona umuhimu huo na kusimamia kwa faida ya kuongeza tija katika
ufundishaji” alisisitiza Dkt.Akwilapo
Awali akiongea kwenye
hafla hiyo Gwen Walmsley alirudia kuipongeza Tanzania kwa juhudi zake
za uboreshaji wa elimu na nchi hiyo itaendeleza ushirikiano kwenye sekta
hiyo ili kuweza kuongeza na kuboresha ufundishaji wa wanafunzi.
Alisema kuwa
wamefurahi kuona mradi huo ukisaidia kuongeza tija kwenye ufundishaji
kwa waalimu kupata vifaa hivyo kwenye vyuo vya ualimu nchini na kuwataka
waalimu kuendelea kutumia vifaa hivyo kuongeza maarifa kuendana na
teknolojia ya Tehama duniani.
Serikali ya Canada
imetoa jumla ya kompyuta 780 kompyuta mpakato 43 mashine za kudurufu
(printers) 74 vitabu 26,470 Photocopy mashines 35 projectors 100 na
dijiti duplicators 35 .
Vifaa hivyo
vilivyokabidhiwa kwa chuo cha Elimu Maalum ya ualimu Patandi kwa niaba
ya vyuo vya ualimu 35 vya serikali ambapo mkuu wa chuo hicho Lucian
Segesela alishukuru kwa niaba yao na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo.
Alisema kuwa vifaa
hivyo vimekuja wakati muafaka na vitasaidia kuongeza uboreshaji wa elimu
nchini na kwa waaalimu tarajali kuongeza ufanisi wa ufundishaji na
kujifunza kwa tija.
Nae Rais wa wanafunzi
wa chuo hicho Engrebert Alex aliishukuru serikali zote mbili na kueleza
kwamba Sasa wanaenda kuvitumia vifaa hivyo kuboresha mazingira ya
ufundishaji kwa wanafunzi nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...