Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya China inayofanya kazi nchini  (Over Seas Chinese  Services Center) imetoa msaada kwa Wananchi waliopata maafa ya mafuriko mkoani Lindi.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Chama cha Msalaba Mwekwendu Tanzania Red Cross wenye thamani ya sh.milioni 30.Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Taasisi ya China Aston Yi amesema kuwa Tanzania ni China ni familia moja hivyo wanajibu wa kutoa msaada kwa wahanga wa maafa.

Amesema kama Taasisi imeguswa na wahanga wa mafuriko mkoani Lindi hivyo kwani baadhi yao wamepoteza kila kitu hivyo japo wapate vitu hivyo.
Aidha amesema wataendelea kuwa pamoja na watanzania pale panapotokea majanga hayo.

Vitu walivyotolewa kwa wahanga wa mafuriko mkoani Lindi ni Nguo 600  Viatu Jozi 360, Unga Kilogram 2350, Vitabu 1250 pamoja na mashuka  mazito 640.

Nae Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana na Majanga wa Tanzania Red Cross Jonston Weston amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa  Lindi wanahitaji msaada kwani baadhi yao wamepoteza makazi.

Amesema kuwa katika elimu wanayoitoa kwa Wananchi ni pamoja kuwataka kufatilia taarifa za mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuchukua tahadhari mapema.
 Mkurugenzi wa Over seas Chinese Services Zhu Jin Feng akimkabidhi vitu mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko mkoani Lindi Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana wa Tanzania Red Cross Jonston Weston  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Moja ya sehemu ya msaada kwa wahanga wa Mafuriko mkoani Lindi uliotolewa na over seas Chinese Services Center.

Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana na Majanga wa Tanzania Red Cross Jonston Weston akizungumza mara baada ya kutokea msaada kutoka kwa Taasisi ya Over seas Chinese Services Center kwa ajili ya wahanga wa  Mafuriko mkoani Lindi.
Mkurugenzi wa Over seas Chinese Services Center Aston Yi akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa wahanga wa Mafuriko mkoani Lindi kwa Tanzania Red Cross
Picha ya pamoja. Kati Tanzania Red Cross pamoja na watendaji wa over seas Chinese Services Center.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...