Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wajasiriamali wanaozalishaji wa bidhaa mbalimbali zinzotumia kemikali wametakiwa kutumia kemikali hizo kwa usalama ili ziweze kuleta madhara kwa watumiaji na wakati mwingine madhara hayo yanaweza kutokea hata kwa wazalishaji.
Akizungumza katika Mafunzo ya wajasiriamali wa Wadogo na Kati wa Kanda ya Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa uchumi wa viwanda nchini pamoja na wazalishaji wa bidhaa wanaotumia kemikali wanahitaji kuwa na matumizi salama ya kemikali hizo.
Dkt.Mafumiko amesema kuwa kemikali zisipotumika kwa usahihi zinaweza kuleta madhara ya kimazingira ambapo athari zake ni kubwa ambapo maendeleo yanayohitajika yasiweze kufikiwa.
Amesema kuwa wananchi wanauelewa wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kwa kutokana na kujisajili vibali vya uingizaji wa bidhaa za kemikali nchini hivyo watumiaji nao lazima wawe na elimu ya utumiaji wa Kemikali hizo katika uzalishaji wa bidhaa.
“GCLA inataka wajasiriamali waendelee ni pamoja na kutumia kemikali kwa usahihi wake ili zisiweze kuleta madhara kwa wananchi kutokana na kutumia bidhaa ambazo kemikali zake hazijatumika kwa taratibu zinazotakiwa”amesema Dkt.Mafumiko
Dkt.Mafumiko amesema kuwa mafunzo mengine yatakwenda kwa wauzaji wa kemikali ambao wanatakiwa kuuza bidhaa za kemikali zilizo bora na si vinginevyo .
Mkurugenzi wa Sabuni za Usafi Majumbani na Viwandani Jovita Masanyika amesema kuwa Mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani ndio watumiaji wa kemikali katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Amesema kuwa elimu walioipata wataitumia katika utengenezaji wa bidhaa bora kwa kuzingatia matumizi salama ya kemikali na kuongeza kuwa wauzaji nao wanatakiwa kupewa elimu hiyo.
Mkufunzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) George Buchafwe amesema kuwa SIDO itaendelea kushirikiana na GCLA katika kuhakikisha wajasiriamali wanafikia viwango vinavyohitajika katika matumizi ya kemikali.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akizungumza katika mafunzo
ya Wajasiriamali wa Kanda wa Mashariki kuhusiana na matumizi sahihi ya
Kemikali yaliyfanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali wa Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) Daniel Ndiyo akitoa maelezo wakati
akiwakilisha mada kwa wajasiriamali wa kanda ya mashariki iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) George Buchafwe
akizungumza namna wanavyowaratibu wajasiriamali katika uanzishaji wa wa
viwanda namana ya kufuata taratibu za serikali.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi
wa habari kuhusiana Mamlaka hiyo inavyodhibiti kemikali nchini zisiweze
kutumika vinginevyo wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa Kanda ya
Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sabuni ya Usafi Jovita Masanyika akizungumza namna
wanavyotumia kemikali katika uaandaji wa bidhaa za sabuni wakati wa
mafunzo kwa wajasiriamali wa Kanda ya Mashariki yaliyofanyika jijini Dar
es Salaam.
Mjasiriamali wa Sabuni Maria Lwila akitoa maelezo kuhusiana na
upatikanaji wa kemikali wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa Kanda ya
Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali wa Kanda ya Mashariki mara baada ya kufungua mafunzo ya kwa wajasiriamali hao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...