Na Khadija Khamis
Mkurugenzi wa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi  Zanzibar  Dkt. Khamis Ali Omar amewataka wananchi kujitahadhari na matumizi ya chakula na dawa  ambazo zimemaliza muda na vipodozi ambavyo havijathibitishwa  ili kuepuka maradhi yatokanayo na sumu .

Hayo aliyasema huko katika Ofisi ya Mkuu wa  Wilaya ya Mjini,  Sebleni wakati akitoa Mafunzo ya usalama wa chakula dawa na vipodozi  kwa Masheha wa Wilaya hiyo  na kuwataka ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha wanathibitisha  matumizi hayo kwa wananchi.

Alisema madhara yatokanayo na matumizi ya chakula dawa na vipodozi ambavyo haviko katika kiwango kuhatarisha afya ya mtumiaji pamoja na kupata madhara makubwa ikiwemo Saratani ya Ngozi .

Aidha aliwataka Masheha kutoa ushirikiano kwa Maofisa hao kwa uingizwaji wa bidhaa za chakula dawa na vipodozi  katika Shehia zao,  bidhaa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi zinazozalishwa  ndani ya nchi na nje ya nchi .

Nae Mkuu wa Ukaguzi Idara ya Uthibiti Usalama wa Chakula Mohamed Shadhil Shomar amesema wanafanya Ukaguzi wa Usalama wa Bidhaa katika Majengo tofauti yakiwemo  Maghala ya Chakula na Vipodozi, maduka ya Chakula Vipodozi na Dawa (OTC)Bekari,Bucha, Mikahawa Vioski, Hoteli, Supermarket na Viwanda pamoja na kufanya ukaguzi katika vituo vya Forodha ikiwemo Bandari ya Mkokotoni,Malindi na Uwanja wa Ndege Kisauni  kwa bidhaa zinanazoingia  .

Alifahamisha kuwa Wakala wa chakula dawa na vipodozi Zanzibar inafanya usajili wa majengo yote yanayotoa  huduma za bidhaa kwa Jamii  ili kuyadhibitisha majengo hayo kwa kuzuiya uzalishaji usambazaji pamoja na uuzaji wa bidhaa za chakula dawa na vipodozi ambavyo havijasajiliwa na ZFDA ,

Kwa upande wa Mkuu wa Ukaguzi Kitengo cha vipodozi Zanzibar Salum Hamad Kassim amewataka wananchi waachane na matumizi ya vipodozi haramu  bila ya kufuata utaratibu jambo ambalo husababisha maradhi ya ngozi .

Alisema vipodozi hutumika kwa njia ya kujipaka katika sehemu ya mwili (Juu ya Ngozi ) kwa kuosha ,kunyunyiza kujipulizia kwa lengo la kujiremba, kujisafisha, kujipamba, kuongeza uzuri wa ngozi na kubadili muonekano wa sura halisi.

Nao Masheha wa Wilaya ya  Mjini wamesema watu sio waaminifu wanatumia njia isio sahihi kwa kuuza bidhaa zao kwa bei ya kutupa  na kujipatia kipato ,bidhaa ambazo tayari zinakaribia kumaliza muda au zimeshamaliza muda wa Matumizi .

“Tatizo ni kubwa mno tofauti na mnavyofikiria kuna saloon tele mitaani ambazo watumizi ni akinamama  madawa ya mikorogo yanayotumika kubadilisha ngozi halisi ya awali pamoja na vinywaji vya alkasusi ambavyo ndio vinavyochangia  vitendo vya upakaji nchini “, walisema masheha hao

Kwa upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Mjini Juma Abdalla Hamad ametoa wito kwa masheha hao kutoa ushirikiano na mamlaka husika kwa lengo la udhibiti wa uingizwaji na uuzwaji bidhaa zisizostahiki kutumika nchini. 

“Kila Sheha awajibike katika Shehiya yake kuweza kuchunguza bidhaa ambazo wanauziwa wananchi wake ahakikishe bidhaa wanazouziwa wananchi zina  usalama wa kutosha na zimethibitishwa kwa matumizi ya binaadamu” .
 Mkuu wa Ukaguzi Kitengo cha Vipodozi Zanzibar Salum Hamad Kassim  akitoa elimu  kwa Masheha wa Wilaya ya Mjini juu ya matumizi mabaya  ya Chakula Dawa na Vipodozi na athari zake huko katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Sebleni
Masheha wa Wilaya ya Mjini wakimsikiliza Mkurugenzi wa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi  Zanzibar  Dkt. Khamis Ali Omar ambae (hayupo pichani ) juu ya matumizi mabaya ya chakula dawa na vipodozi kwa jamii huko katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Sebleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...