Mfanyabiashara mkazi wa Malapa Aisha Ally akifanya maalipo baada ya mizani yake kuhakikiwa na Afisa Vipimo Clement Costantino.
 Mkazi wa Buguruni Victor Kelei akihakiki mizani yake eneo la ofisi ya Kata ya Buguruni Mtaa wa malapa.
Mafundi wakitengeneza au kurekebisha mizani yenye hitilafu Kata ya Buguruni Mtaa wa malapa.

WAKALA wa Vipimo mkoa wa Ilala  umewataka wafanyabiashara wanaoagiza ama kuuza mizani mipya kuhakikisha mizani hiyo imehakikiwa na Wakala wa Vipimo kwa mujibu wa sheria.

Wito huo umetolewa leo Februari 28, 2020 na Kaimu Meneja wa Wakala wa  Vipimo wilaya ya Ilala,  Malaki Nyangasi walipokuwa wakifanya ukaguzi  na uhakiki wa vipimo vinavyotumika katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa mbalimbali katika eneo la  kata ya Buguruni,  mtaa wa Malapa ili kujiridhisha iwapo vipimo  vipo sahihi kwa mujibu wa sheria ya Vipimo sura ya 340, mapitio ya mwaka 2002 na kanuni zake.

"Majukumu ya Wakala ni kuhakikisha Vipimo vinavyotumika kwenye biashara na huduma mbalimbali ikiwamo Afya usalama na mazingira ni sahihi ili kuilinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na matokeo ya vipimo visivyo sahihi ili katika kusimamia matumizi sahihi ya Vipimo wafanye uhakiki na ukaguzi wa vipimo wa mara kwa mara ili kumlinda mlaji". Amesema Nyangasi.

Ameongeza kuwa kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na kuuza mizani mipya, wahakikishe mizani wanayoiuza imehakikiwa na wakala wa vipimo kwa mujibu wa sheria  ya vipimo na kanuni zake na kwa upande wa mnunuzi ahakikishe mizani anayonunua imehakikiwa na wakala wa vipimo kwa kuwa na alama za kugongwa muhuri, stika na  lakili kwa mizani ya kielektroniki.

Nyangasi amesema kwa mfanyabiashara  atakayetumia vipimo visivyo sahihi  na ambavyo havijahakikiwa akibainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kutozwa faini ama kufikishwa mahakamani kwa kutenda  kosa la jinai ambapo adhabu yake ni kutozwa faini isiyopungua Sh 100,000 mpaka Sh. milioni 20.

Nakuongeza kuwa iwapo akipelekwa mahakamani akapatikana na hatia katika kosa la kwanza atatozwa faini isiyopungua Sh 300,000 na isiyozidi Sh 50 milioni ama vyote kwa pamoja.

Katika kosa la pili adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 5 ama faini isiyopungua Sh 100 milioni ama vyote kwa pamoja.

Alibainisha kuwa sekta mbalimbali zinazohusu uzalishaji, biashara na uchumi hutegemea Vipimo sahihi, ili kujua mchango wa kila sekta katika pato la taifa kwa ujumla wake.

Katika kata ya Buguruni  mtaa wa Malapa wafanyabiashara  257 wanaotumia  vipimo walijitokeza kuhakiki mizani yao kwa mwaka 2020.

Kwa upande wa mkazi wa Buguruni Victor Kelei  ambaye alipeleka mizani yake kuhakikiwa alisema hatua hiyo imekuwa ikiwasaidia kufanya biashara zao kwa uaminifu na kuondoa lawama kwa wateja kwa kuwa wanapata huduma kulingana na kiasi cha fedha walichotoa.

Mkazi wa Malapa, Aisha Ally ambaye naye alipeleka mizani yake kuhakikiwa aliwahamasisha wafanyabiashara wanaotumia mizani kuhakikisha inahakikiwa 2020 ili kutoa huduma kwa wateja wao kwa uaminifu na kuwavutia waendelee kufika katika biashara yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...