Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akipokea maelezo ya ujenzi wa mradi
kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa mradi wa maji wa Tabora,
Igunga, Nzega na Uyui wakati wa ziara yake kwenye mradi huo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelekezo kwa wakandarasi
wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui
wakati wa ziara yake kwenye mradi huo.

Ujenzi ukiendelea kwenye moja ya eneo la mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua na kutoa maelekezo ya
utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui
………………………………………………………………………………………………………..
Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amewataka wakandarasi
wanaojenga mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega, Uyui na Tabora
kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili ukamilike kwa wakati.
Mhandisi
Sanga ametoa maelekeo hayo Mkoani Tabora Februari 4, 2020 wakati wa
ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji mkoani
humo.
Mara baada ya
kutembelea eneo la mradi huo na kujionea hatua iliyofikiwa, Mhandisi
Sanga alizungumza na wakandarasi wanaoutekeleza ambapo alieleza
kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa.
Hata hivyo,
licha ya kuridhishwa na ubora wa ujenzi wa mradi, Mhandisi Sanga
aliwataka wakandarasi hao kuelekeza nguvu zaidi kwenye kazi
zinazopelekea wananchi kupata maji kwanza badala ya kuweka nguvu kubwa
kwenye maeneo mengine.
“Pamoja na
kazi nzuri inayoonekana kufanyika maaelekezo yangu ni kuwa wakandarasi
wote mhakikishe kuwa kazi zinazofanyika kwa sasa ni zile ambazo wananchi
wataanza kupata maji mapema iwezekanvyo badala ya kuweka nguvu kwenye
majengo na mambo mengine,“ alisisitiza Mhandisi Sanga.
Alibainisha
kuwa wananchi wamesubiri mradi huo kwa muda mrefu na kwamba kwakuwa
tayari kumefanyika kazi kubwa wahakikishe maeneo machache ambayo bado
hayajakamilika wanayakamilisha.
“Mnapaswa
kuelewa wananchi wameusubiri mradi huu kwa muda mrefu, hizi kazi
zilizobakia mhakikishe zinakamilika haraka, shughuli zingine kama kupaka
rangi majengo zitafanyika baada ya kuwa tayari wananchi wanapata
huduma,” aliongeza Mhandisi Sanga.
Kwa upande
wao Wakandarasi hao walimhakikishia Naibu Katibu Mkuu kutekeleza
maelekezo aliyoyatoa na waliahidi kuhakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi
wa mradi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi hadi muda wa ziada ili tu
inapofika Februari mwishoni maji yawe yamefika kwenye maeneo yote
yaliyokusudiwa ya Tabora mjini, Nzega, Igunga na Uyui.
Mradi wa maji
wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui unajengwa na Kampuni tatu kutoka India
ambazo ni Megha Engineering Infrastructures, L&T na Afcons kwa
gharama ya shilingi Bilioni 602 zikiwa ni fedha za mkopo kutoka benki
ya Exim ya India.
Mradi huo
unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 30 kutoka Agosti 2017 na unatakiwa
kukamilika tarehe 23 Februari, 2020 kwa mujibu wa mkataba na kwamba
kukamilika kwake kutawezesha jumla ya wananchi 1,200,000 kunufaika na
huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...