Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wafanyabiashara wadogo (machinga)kuacha kufanyabiashara kwenye maeneo ya mahakama kwa kuwa wanazuiya njia wananchi wanaenda mahakamani hapo kwa shughuli za mahakama.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wafanyabiashara wadogo (machinga)kuacha kufanyabiashara kwenye maeneo ya mahakama kwa kuwa wanazuiya njia wananchi wanaenda mahakamani hapo kwa shughuli za mahakama.
Na kuagiza wanaofanyabiashara maeneo hayo kuona umuhimu wa kuyaachia Mara moja ili kuifanya mahakama kufanyakazi zake kwa utulivu na kuondoa adha kwa wananchi wenzao kwa kuwa hakuna mhimili usio na faida yote ipo kwa mujibu wa sheria hivyo tufanyekazi kwa kuheshimu sheria kwa kuwa wote tupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Kwa muktadha huo akatoa angalizo kwa viongozi wa wamachinga wanaofanya biashara kwenye maeneo ya mahakama kukaa pamoja na viongozi wa mahakama na mkoa kuainisha maeneo ya mahakama ili kuona namna nzuri ya kuondoka katika maeneo hayo ya mahakama kwa wafanyabiashara hao bila kusukumana.
Agizo hilo amelitoa kwenye siku ya sheria na mwaka wa mahakama iliofanyika jijini Arusha ambapo alisema kuwa atakaa na watendaji wa mahakama viongozi wa wamachinga kuona namna nzuri ya kupanga ili kuwezesha shughuli za mahakama kufanyika bila bughudha.
Kwa mujibu wa Gambo aliwataka Mahakimu wote kutenda kazi kwa kufuata kanuni tusicheleweshe Wala kuahirisha kesi za wananchi kwani zinaongeza gharama kwa kutojua mwananchi ametoka umbali gani.
Alieleza kuwa Elimu ya sheria na adabu za mahakama zinatakiwa kutolewa kwa wananchi ili kuondoa changamoto kwa wananchi kupata adha ambazo zinaepukika kwa kutumia muda mfupi wa kushughulikia mashauri mapema na kuangalia Jambo lenyewe ili kuongeza utoaji haki.
“Tutumie utu na kujali dhamana tulizopewa kwa lengo la kutumia madaraka
yetu vizuri,angalieni changamoto ya utoaji wa nakala za hukumu ili kuondoa
kero na adha kwa wananchi wetu, tuangalie jinsi ya kuondoa vitendo vya
kihalifu kwa kutumia sheria zilizopo kwa kuwa wakweli,pia kumekuwa na
changamoto za kubambikiwa kesi na ucheleweshaji wa mashtaka nendeni
mkaliangalie hayo”alisema Gambo
Alisema kuwa haki inayocheleweshwa iangaliwe ili kuondoa kero kwa kutumia muda na kutocheleweshwa kwa kesi na hivyo wananchi kutopata haki yao kwa wakati kwa kila moja kutimiza wajibu wake katika mashauri yanayoletwa mahakamani,hivyo viongozi tuheshimu mihimili iliyopo ili kuwafanya wananchi kuheshimu sheria na mahakama.
Kwa Upande wake Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha Mosses Mzuna alisema kuwa watumishi wajipambanuwe kwa lengo la kutoa haki kwa wakati kuendana na dhumuni kubwa la sheria ni kuhamasisha mahusiano ya biashara.
Alisema kuwa uwekezaji wa kibiashara ni kutega fedha au uchumi ndio maana mahakama ikaona umuhimu kuiweka katika kauli mbiu yake ya mwaka huu ili uwekezaji na mazingira wezeshi iwe sehemu ya utoaji haki na sehemu ya mahakama.
“Sheria zetu hazipo mbinguni zipo duniani hivyo mahakama iende na kuangalia masuala ya kiuchumi ili ziweze kuendelea, kwa kuenda sambamba na utoaji haki kwa kuharakisha migogoro ya kibiashara kwa lengo la kuvutia wawekeza ambao wataweka mitaji mikubwa kwa kuwa watakuwa na Imani na mahakama zetu”alieleza Jaji Mzuna akisoma nukuu ya Rais mstaafu Mkapa
Alisema mahakama kama hazitachelewesha mashauri na kutoa haki kwa wakati hakika ongezeko la Masha Bora jamii inayopenda kujifunza zaidi amani na utulivu nasi kama mahakama hatuwezi kujitenga kwenye sera hiyo kwa kushirikiana na wadau.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...