Na.Catherine Sungura-Uvinza
Wananchi
wa kijiji cha Kalenge wilayani hapa wameishukuru Serikali ya awamu ya
tano kwa kuwajengea zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na
uzazi.
Hayo yamebainishwa jana na wakazi wa
kijiji hicho wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Dkt.
Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya usimamizi shirikishi mkoani kigoma
ambayo inafanywa na wizara ya afya pamoja na TAMISEMI.
Akiongea
kwa furaha bi. Marystela Chishako alisema kuwa wanaishukuru serikali ya
awamu ya tano kwani kwa kupata zahanati hiyo imewasaidia kupata huduma
za afya ikiwemo huduma ya kujifungua ambayo awali walikua wakiifuata
kigoma mjini.
"Tunashukuru kwa serikali hii
kutukumbuka mkoa wa kigoma,siku za nyuma mama akitaka kujifungua ilibidi
aende kigoma mjini,ila hivi sasa tunajifungulia hapa hapa kwenye
zahanati na tunapata huduma muhimu hapa hapa".
Aidha,
alisema zahanati hiyo imewasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto
kwani kipindi cha nyuma walikua wakipata matatizo njiani kwa sababu
walikua wakisafiri umbali mrefu na kupelekea kupata matatizo wakiwa
njiani.
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu
Dkt.Chaula aliwahidi kulifanyia kazi ombi lao la kupatiwa kituo cha afya
kwani wameshaomba kwa kufuata utaratibu kupitia mkoa.
"Ninawapongeza
kwa sababu mmejua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya,kwahiyo maombi
yataletwa wizara ya afya kutoka TAMISEMI,na katika ziara yangu
nimeongozana nao hapa na nimepokea ombi hili najua ukitoa ahadi lazima
utimize".Alisema Dkt. Chaula
Hata hivyo Katibu
Mkuu huyo amesema atahakikisha wanapata fedha ili kutimiza ndoto za
wananchi hao"mmefanya wajibu wenu na uzalendo mkubwa wa kuipenda nchi
yenu kwa kujituma mpaka mmetenga eneo na kuweka mawe na mchanga, hivyo
serikali itaongezea nguvu pale mlipoanzisha.
Wakazi
wa kijiji hicho wametenga eneo la hekari ishiriki,kukusanya mawe pamoja
na mchanga kwa kujitolea ili kuweza kujenga kituo cha afya ikiwa ni
juhudi za kuiunga mkono serikali kwa kutatua changamoto za huduma za
afya karibu na wananchi.
Jengo la kujifungulia ambalo limejengwa katika zahanati hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto-Idara kuu Afya Dkt.Zainab Chaula akisalimiana na mmoja wa
watumishi wa afya wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza mara ya kufika
kwenye zahanati ya kelenge
Mkurugenzi wa idara ya tiba Dkt. Grace Magembe akiongea na wakazi wa kijiji hicho,kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto-Idara kuu Afya Dkt.Zainab Chaula
Mkazi wa Kelenge Jonas Kabwelega akiongea mbele ya katibu mkuu jinsi walivyojipanga kujenga kituo cha afya kwenye kijiji hicho
Wakina
mama wa kijiji hicho wakiimba kwa furaha mara ya kuahidiwa kujengewa
kituo cha afya ambacho kitasogeza huduma za afya kwenye kijiji
hicho(Picha zote na Catherine Sungura)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...