Na Amiri kilagalila,Njombe
WANANCHI wa kijiji na kata ya Ibumi wilayani Ludewa mkoa wa Njombe  wamejitokeza kwa wingi wakiwa na zana za mikono kwenda kurekebisha barabara ya kutoka Ibumi kuelekea Ludewa mjini.

Barabara hiyo inayounganisha kata za Ibumi na Ludewa imeharibika zaidi katika eneo la mlima Nyamikuyu na eneo la mto ketewaka na madenge hasa katika kipindi hiki cha masika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Zoezi la harambee ya kurekebisha barabara hiyo kwa kutumia majembe, sululu na chepe liliongozwa na diwani wa kata ya Ibumi ambae ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mhe, Edward Haule na mwenyekiti wa kijiji cha Ibumi Bw, Oscar Komba.

Baadhi ya wadau wenye vyombo vya usafiri katika kijiji cha Ibumi walitoa magari yao kwaajili ya kusafirisha wananchi hadi eneo la kazi pamoja na kusomba kifusi kilichotumika kuweka katika maeneo korofi.

Wananchi wa kijiji hicho wamesema Barabara hiyo ni muhimu kwakuwa imekuwa ikitumika kila wakati na wananchi wa kata hizo mbili ambao kwa asilimia kubwa ni wakulima wa mazao ya chakula na biashara pia inaunganisha mkoa wa Njombe na Ruvuma hivyo wanaiomba Serikali kupitia (TARURA) kuboresha maeneo hayo.

“Barabara hii ni Muhimu sana maana inaunganisha mkoa wetu wa Njombe na mkoa jirani wa Ruvuma kupitia kata yetu ya Ibumi pia inaenda hadi yaliko madini ya chuma cha Liganga kule Mundindi hivyo, tunaomba Serikali itambue kazi yetu” wameeleza wananchi hao.

Diwani wa kata ya Ibumi, Edward Haule amesema kazi hiyo ni endelevu, hivyo amewaomba wadau na wananchi wa Ibumi walioko nje ya kata hiyo kuchangia japo fedha kwaajili ya chakula na mafuta ya magari ili kuunga mkono nguvu za Wananchi ambao wameamua kujitoa kufanya kazi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...